BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, April 14, 2010

MTU SABA KUISIMAMISHA WANAUME HALISI BAADA YA KIMYA KIREFU!

Kundi la TMK HALISI limesaini mkataba na kampuni inayoitwa DLC ambayo inafanya biashara zake China na Tanzania, kampuni hii ambayo yenyewe ndiyo itasimamia kila kitu ikiwemo mambo ya promosheni kutafuta maonyesho ya nje na ndani ya nchi pia kusimamia mauzo ya kila kitu.

Kiongozi wa kundi hilo Juma Kassim Nature, amepata wakati mgumu sana kuchuja na kuchagua vichwa vinne atakavyo fanya navyo kazi ya kuunda TMK Halisi mpya yenye vichwa vitani akiwemo yeye...badala ya ile ya awali iliyokuwa na wasanii 12.

Walio chaguliwa kusaini mkataba huo ni DOLO, BABA LEVO,JB WA MABAGA FRESH,KG SON pamoja na Juma Nature mwenyewe.

Tayari kundi hilo linalodhamiria kurudi upya baada ya kufulia kwa muda wa kutosha katika anga ya muziki wa kizazi kipya,limeshafanya kazi inayoitwa MNATAKAJE? ambayo imeanza kusambazwa redioni tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment