BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, April 22, 2010

TANGA FLAVA YAPIGA HATUA!!

Hatimae wasanii wa Tanga ambao wanafanya muziki wa Bongo Falva wamepata unafuu wa nyimbo zao kujulikana baada ya blog hii kuwatengenezea Playlist.

Sasa unaweza kusikiliza nyimbo za Tanga Flava kupitia Blog hii kwa kubonyeza wimbo wowote ule unaoutaka hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!

Hii itawasaidia wasanii wa Tanga kufahamika zaidi ndani ya Tanga, Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Tumeanza na nyimbo chache hapo juu lakini nyingi zaidi zinakuja.

Nyimbo ambazo zipo kwenye playlist ni Mr President (Roma), Asali Shubiri (Fady Dady), Njoo Basi (Mo Kweli ft Mkolini), Aisha (Bwi Bwax), Ulisema (Shomy Love ft Big Smart), Taswira (Mwandei), Samahani (Pete), Mungu Yuko Bize (Bwana Misosi ft Chegge), Kila Sehemu (Omega Boys), Masham Sham (Dr John), Niite Mimi (Mitago ft Timer), na Nenda (Pete ft Tanga Stars)

Sikiliza ladha za wasanii wa Tanga.



No comments:

Post a Comment