BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, April 1, 2010

PANGANI MPAKA KIELEWEKE!

Leo asubuhi wananchi wa Pangani walishindwa kufanya shughuli zao za kawaida kwa wale wanaovuka ng'ambo baada ya kivuko kinachofanya kazi ya kuvusha watu kushindwa kufanya kazi. Kivuko hiki kimekuwa kero sasa kwa wananchi wa Pangani!!!

Hapa kikiwa kimeelemewa na kutoka kabisa katika njia ya kushushia abiria. Mbaya zaidi kinatumia injini moja hivyo usafiri kuwa wa mashaka mpaka kufika ng'ambo ya pili.

Kikiwa juu ya mawe! Hilo gari baada ya kuingia tu kivuko hicho kilishindwa kuendelea na safari na badala yake kubakia hivyo mpaka sasa.

Hapa wananchi wa Wilayani Pangani wakivuka kwa kutumia vidau baada ya kivuko cha MV Pangani kuharibika leo asubuhi huku kivuko kipya ambacho kipo tayari kikidaiwa kusubiri kuzinduliwa na Rais Kikwete

Wananchi wakiwa katika foleni ya kuvuka.

Kivuko kikiwa ju ya mawe baada ya kushindwa kufanya kazi.

Ombi! Tunakuomba Mh Rais Jakaya Kikwete uje utufungulie hiki kivuko kipya kwani tumesikia kipo tayari na huenda kingefunguliwa rasmi mwezi wa tatu!

No comments:

Post a Comment