BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, April 20, 2010

MAANDAILIZI YA MISS CHUMBAGENI NI MOTO!!!

Punde tu baada ya mashindano ya Miss Tanga kuzinduliwa, tayari waandaji wa miss vitongoji wameanza mchakato wa kuhakikisha wanapata warembo ambao wataingia moja kwa moja kunako kambi ya kumsaka mnyange wa Miss Tanga. Kitongoji cha Miss Chumbageni ni moja ya vitongoji ambavyo vipo kwenye mchakato huo ambapo juzi walikutaka kwenye ukumbi wa La Club Tanzanite kwa ajili ya maandalizi. Pichani Julieth Kulangwa ambaye ndie muandaaji mkuu wa Miss Chumbageni kupitia kampuni ya Apple Partners Group.

Align CenterMdau wa urembo jijini Tanga, Blandina Lukindo ambaye pia ni mtangazaji wa redio Mwambao Fm akiwa katika pozz wakati wa mazungumzo ya kuandaa Miss Chumbageni.

Warembo katika mjadala wa kutafuta vichuna wa Miss Chumbageni.

Mambo yalikuwa mazito lakini tamati ilikuwa nzuri. Tayari Miss Chumbageni ina warembo tisa ambao watapanda juu ya stage kuumana vikali siku ya Mei Mosi tarehe 1/may/2010 Jumamosi.

Mtangazaji mwengine wa Mwambao Fm dada Neema Inana akiwa makini kwenye kikao.

Dada Suzane Uhinga, mmoja kati ya waandaji wa Miss Chumbageni kutokea kampuni ya Apple Partners Group akionyesha tabasamu pana wakati wa kikao.

Swahiba wangu wa ukweli Bra A alikuwepo.

Hapa no Comment kwa Blandina Lukindo, sijui alikuwa anataka kurembua maana hata sijaelewa. Ila hako kabinti pembeni 'DOLE TUPU'

No comments:

Post a Comment