Rais wa Eckenford Tanga University ndugu Amos Fide akizungumza wakati wa kuwakaribisha wanafunzi wa chuo cha Sekuko kutokea wilayani Lushoto wakati wanafunzi wa chuo hicho walipokuja jijini Tanga kwa ajili ya kuwatembelea wenzao pamoja na kucheza michezo ya kirafiki ya mpira wa miguu pamoja na netball.
Mwalimu wa chuo cha Sekuko ndugu Mtoi Philimon aliyekunja mikono akiwa na mwenyeji wake ambaye pia ni rais wa chuo cha Eckenford Tanga University Amos Fide wakati wa utambulisho ulifanyika chuoni hapo kabla ya kuelekea Mkwakwani kwa ajili ya michezo ya kirafiki. Mimi unaniona kwa hapo nyuma, nilikuwa mgeni mwalikwa kutoka kwa rais wa chuo.
Hapa tukipata picha ya pamoja na viongozi wa vyuo vyote viwili.
Hapa nikiwa na Amos Fide rais wa Eckenford Tanga University tukitazama mchezo wa netball na kubadilishana mawazo
Wanafunzi wakittazama mchezo wa netball ambapo timu ya chuo cha Eckenford kiliibuka na ushindi wa magoli 22 kwa 6
kazi ikawa huku sasa! Hawa ni wachezaji wa timu ya chuo cha Eckenford.
Shangwe za kushangilia zilikuwepo
Picha ya pamoja tena na viongozi wa Eckenford Tanga University tukiwa Mkwakwani.
Kila mtu huvuta hisia anapovutiwa na mchezona
Kikosi cha timu ya chuo cha Sekuko kutoka Lushoto
Kikosi cha Eckenford Tanga University
Hapa kilikuwa ni kipindi cha mapumziko ambapo kwa kipindi hicho cha kwanza Sekuko iliibuka kwa magoli 2-0
Eckenford Tanga University wakijaribu kujadiliana katika kipindi cha kwanza. Hata hivyo walishindwa kufurukuta mbele ya Sekuko kwani mpaka dakika tisini walilazwa kwa jumla ya magoli 4-0
No comments:
Post a Comment