BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, July 1, 2011

MASHINDANO YA POOL TABLE MKOANI TANGA KUANZA JULAI 7

Msimu wa mashindano ya kutafuta klabu bingwa ya mchezo wapool mkoani tanga umeanza, pichani ni meneja wa bia ya safari lager mkoani tanga mr. mbise (kushoto) akiwa na katibu mkuu wa chama cha pooltable mkoa wa tanga (tarpa) shaban kibelloh wakiwa katika ukumbi wa hoteli ya ze city kulikokuwa na 'speed pool'Wataalam wa kampuni ya intergreted ya jiji dar es salaam inayohusika na matangazo ya bia ya safari lager wakitoa matangazo yao kuhusu kuanza rasmi kwa mashindano ya pool mkoani tanga.


Katika msimu huu wa mashindano ya pool kulikuwa na shindano dogo la kutafuta bingwa anayeweza kuingiza kete zote 15 ndani ya dakika 3 tu na pichani ni bingwa aliyeweza kuingiza kete hizo kwa kutumia dakika 2 na sekunde 32 huyo si mwingine ni ally shariff mchezaji wa klabu ya kwaminchi. hii ni speed pool


Hapa mshindi wa speed pool ally shariff akiwa na mtangazaji wa intergreted bi latifa mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake kisha kuvalia jezi yake ya safari lager hapa akiongea maneno mawili matatu na latifa.
Picha zote na Mashaka Mhando

No comments:

Post a Comment