BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, July 18, 2011

TIMU YA DALADALA ILIVYOFANYA KAZI YA KUREKODI VIPINDI MKOANI TANGA

Tayari timu nzima ya kipindi cha daladala kimeshafanya baadhi ya vipindi mkoani Tanga, ambapo vipindi hivyo utakuja kuviona kwa luninga yako kupitia televisheni ya ITV kila siku kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa moja jioni.

Maswala mbali mbali kuhusiana na mgao wa umeme, maendeleo ya bandari ya Tanga- wananchi wanaionaje. Swala la elimu na mmomonyoko wa maadili pia vimezungumziwa katika moja ya vipindi vilivyorekodiwa na timu ya daladala iliyotua jijini Tanga.

(Pichani mimi na Daniel Kijo, mtangazaji wa kipindi cha daladala)

Nikiwa mmoja wa watu walioshiriki kutoa maoni mbalimbali katika kipindi cha daladala, kwa kweli katika mijadala yote niliyoishuhudia wakati wa kurekodi vipindi- wananchi wa mkoa wa Tanga wameonyesha ushirikiano wa kutosha na wengi wamezungumza kwa hisia kwa kile ambacho kilikuwa kinawagusa moja kwa moja.

(Pichani Daniel akiwa na mdau wa kipindi cha daladala, barabara ya nane)

Safari ilianzia Mwahako mpaka eneo la stendi ambapo walipanda abiria wengine na mjadala kuendelea. Badae tena daladala ilikwenda eneo la Magomeni na kisha wanafunzi wa chuo kikuu cha Tanga cha Eckenford nao walipata nafasi ya kutoa maoni yao pia kuhusiana na swla zima la elimu huku bwana Kombo ambaye ni afisa wa elimu ya sekondari wilaya ya Mkinga akiwa chachu ya mada hiyo.

(Timu ya kipindi cha daladala wakiwa na afisa elimu Kombo wakati wa kuelekea kurekodi)

wananchi wa Tanga wakae mkao wa kula kutazama vipindi vilivyotengenezwa kutokea hapa Tanga kuanzia leo tarehe 19 siku ya jumanne kuanzia saa kumi na mbili na nusu mpaka saa moja kujua mengi kuhusiana na mkoa wa Tanga.

(Daniel kwenye bustani za Tanga)

Eldad Mark Film Director akiwa na Deogratius Sizya Camera man wa kipindi cha Daladala pamoja na afisa wa elimu za sekondari wilaya ya Mkinga Bwana Kombo wakijiandaa na mahojiano.

Kipindi cha daladala pia kilikutana na rais wa Eckenford Tanga University bwana Amos Fide na kufanya nae mahojiano. Pichani ni Daniel Kijo, Eldad Mark pamoja na Fide.

Vijana wa Kazi.

Mimi nikiwa na Bibi Kiroboto. Bibi mcheshi huyu sijapata kuona. Hapa tukiwa Tanga Televisheni kwa ajili ya mahojiano na kuwapa taarifa wananchi wa Tanga juu ya ujio wa daladala. Ukiiona tu, unakimbilia na kupata kisha ukifika ndani unatoa maoni yako!! Daladalaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Daladala ni kila kona bwana! Hapa ni katika kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh. Bibi kiroboto akiwa na dereva wa daladala bwana Emanuel Zing pamoja mwenyeji wetu bi Winfrida Magawa aliyesimama.

Daniel Kijo akibadilishana contacts na baadhi ya wakuu wa kiwanda cha Tanga Fresh

Mazungumzo ya hapa na pale pia yalikuwepo tulipofika Tanga Fresh.

Daladalaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!

Kwa mbali daladala ikionekana na jengo kubwa la kiwanda cha Tanga Fresh

Tulifika pia Eckenford Tanga University.

Huyu mama alitupa raha sana! Alistaajabu alipomuona bibi Kiroboto. wacha amkumbatie bwana! Raha kuwa na daladala!

Baadhi ya wanafunzin wa Eckenford Tanga Univertisty wakibadilishana mawazo za timu ya daladala.

Wanafunzi wa chuo kikuu cha Eckenford Tanga

Wanafunzi wakiingia kwenye daladala

(Timu nzima ya Daladala iliyokuwepo jijini Tanga ni pamoja na Dani Kijo na Bi Kiroboto ambao ni watangazaji. Wengine ni Eldad Mark Film Director, Emanuel Zing Driver, Deogratius Sizya Camera man, Tanya creative producer, Anton second driver na Steve Martin researcher.)

No comments:

Post a Comment