BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, July 4, 2011

KILELE CHA TAMASHA LA FILAMU TANZANIA- JB AITEKA TANGA!! KUFANYA FILAMU MOJA NA WAZAWA

Jumamosi ilikuwa ni shangwe na furaha kubwa kwa wakazi wa jiji la Tanga pale waliposhuhudia kikomo cha Tamasha la Filamu Tanzania lililokuwa likifanyika katika viwanja vya Tangamano huku likipewa udhamini mnono wa kinywaji cha Grand Malt chini ya Sofia Production ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo kubwa. Katika tamati ya Tamasha hilo alikuwepo msanii mashuhuru nchini JB ambaye hivi karibuni alinyakua tuzo kule Zanzibar kwenye ZIFF kupitia fialmu yake ya Senior Bachelor. Punde tu alipopanda jukwani baada ya kukaribishwa rasmi, JB aliwasabahi wakazi wa Tanga na kuwashukuru kwa ujio wao katika Tamasha hilo. Pia kikubwa aliwaahidi kucheza filamu jijini Tanga na wazawa. Hata hivyo katika tamati ya tamasha hilo kulionyeshwa filamu yake ya Senior Bachelor ambayo kwa hakika ilifurahiwa na watu wengi.
Aliposhuka jukwaani alilakiwa na umati mkubwa wa watu huku kila mmoja akitaka kmpa mkono.


Hapa JB akionyesha upendo wa kutosha kwa mashabiki wake, alizunguka kila kona na alisalimiana na kila mtu.


Raha! Mimi nikiwa na Asmah Makau wa Clouds Fm......
Hili ni gari la kampuni ya Five Brothers Entertainment ambayo inafanya kazi ya kutoa burudani hapa jijini Tanga. Muziki wa uhakika kutoka kwao ndio ulikuwa ukisikika katika Tamasha Hili. Jamaa wamejipanga na wapi safi.

Mkurugenzi wa kampuni ya Five Brothers Entertainment bwana Nassor Makau akiwa na Asmah Makau, ni mtu na dada yake hawa.


Msema chochote siku hiyo alikuwa ni Rass Bizo kutoka Nyakubi Inc, hapa akimkaribisha JB kwa stage!


Rass Bizo kutoka Nyakubi Inc


Kundi zima la Tanga Stars ndio lilikuwa likitoa burudani safi ya taarab.


Musa Kissoki Mkurugenzi wa Sofia Production aliyevaa shati jekundu akibadilishana mawazo na JB na mdau mwengine wa filamu nchini.


Huduma ya Grand Malt ilikuwa ni bure kwa wadau tuliofika hapo.


Timu nzima ya Sofia Production ilikuwepo kuhakikisha inapata kumbukumbu nzuri.Mpiga picha kutoka Sofia Production akiwa na Aisha, huyu ndio mama Sofia Production mwenyewe mke wa Musa Kissoki Mkurugenzi wa Sofia Production ambaye pia anamiliki kampuni ya mavazi hapa jijini Tanga ya Kokoliko Model.


No comments:

Post a Comment