BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, July 14, 2011

KAMPUNI YA TANGA CEMENT YAZINDUA KAMPENI YA UHAMASISHAJI WA UPIMAJI VVU KWA WAKAZI WA PONGWE, TANGA.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya saruji Tanga, David Lee (kulia) akitolewa damu kupima virusi vya ukimwi wakati wa usinduzi wa kampeni ya uhamasishaji kuhusu ugonjwa wa HIV/AIDS iliyoandaliwa na kampuni hiyo kwa wakazi wa mji wa Pongwe mkoani hapa. Anayemtoa damu ni muuguzi kutoka hospitali ya Bombo, Immaculata kadaga

Mkazi wa Pongwe mkoani hapa, Zainabu Hamza akipewa ushauri nasaha kuhusu ugonjwa wa ukimwi mara baada ya kupima damu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji iliyoandaliwa na kampuni ya saruji ya Tanga katika mji wa Pongwe. Anayetoa ushauri ni muuguzi kutoka hopotali ya Bombo Elizabeth Lawuo.


Mkazi wa Pongwe , Selina Anthony akipima virusi vya ukimwi.

Hadija Rashidi kutoka Pongwe nae akipima VVU huku mapaparazi wakifuatilia kwa makini tukio hilo.

No comments:

Post a Comment