BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, July 14, 2011

KIPINDI CHA DALADALA KINAKUJA TANGA!! KAA TAYARI

Daladala ni kipindi kinachorushwa na ITV kila siku jioni saa kumi na mbili na nusu hadi saa moja jioni, kinatarajiwa kuwa jijini Tanga siku ya Jumamosi ya tarehe 16/07/2011 na kuanza kazi Jumatatu hadi Jumanne ambapo Jumatarudi Dar es salaam.

Katika kipindi hicho ambacho abiria (hawalipi nauli) hupata fursa ya kujadili na kutoa hisia zao na maoni yanayogusa maisha yao ya kila siku. Kikiwa jijini Tanga, kipindi cha daladala kitaruhusu mada mbalimabali zinazohusu masuala ya Tanga kama vile ya kijamii,kibiashara na utamaduni.

Timu ya Daladala itakayokuwa jijini Tanga na kuzungumza na wakazi wa Tanga ni Dani Kijo na Bi Kiroboto ambao ni watangazaji. Wengine ni Eldad Mark Film Director, Emanuel Zing Driver, Deogratius Sizya Camera man, Tanya creative producer, Anton second driver na Steve Martin researcher


No comments:

Post a Comment