Filamu ya Senior Bachelor imepangwa kufunga pazia la wiki ya maonyesho ya wazi ya filamu yanayoendelea katika viwanja vya Tangamano mjini hapa. Filamu hiyo ambayo itaonyeshwa jumamosi hii ya tarehe 02/07/2011 katika tamasha la Grand Malt la wazi la filamu linaloendelea ikiwa imeongozwa na Single Mtambalike (Richie) na production manager ni Saidi barafu.
Akiongea na Blog hii Musa Kissoki ambaye ni Mkurugenzi wa Sofia Production waandaji wa Tamasha hilo amesema kuwa anaamini filamu itasisimua wengi kwenye maonyesho hayo hasa kutokana na uigizaji wake.
"JB ni moja ya waigizaji wenye mbwembwe sana, hivyo hii imetoka kuwa moja ya kazi zake nzuri ambazo tutazionyesha katika tamasha hili la Grand Malt la wazi la filamu Tanzania" Alisema Kissoki.
No comments:
Post a Comment