BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Friday, July 15, 2011

KLABU YA COASTAL UNION YA TANGA ILIVYOPATA VIONGOZI WAPYA

Mwenyekiti Mpya Wa Klabu Ya Coastal Union Ahmed Hilal 'Aurora' (Wa Pili Kushoto) akiwa baadhi ya wanachama akiwemo Kitwana Manara (Kushoto Kwake), Steven Mghuto, Albert Peter Na Mwenye Kanzu Ni Alyekuwa Mwenyekiti Wa Klabu Hiyo Kamati Ya Muda Mzee Talhata

Mwenyekiti Mpya Wa Klabu Ya Coastal Union (Kushoto) Akivalishwa Kitambaa Chekundu Na Mmoja Ya Wanachama Wa Siku Nyingi Wa Klabu Hiyo Micheni Ahmed Micheni Baada Ya Kutangazwa Kuwa Mshindi Kisha Mwanachama Huyo Kumpongeza Kwa Kumvika Kitambaa Hicho.

Viongozi Wapya Wa Klabu Ya Coastal Union Waliochaguliwa wakiwa kwenye Makao Makuu Ya Klabu Hiyo Baraara 11 Jijini Tanga, Kutoka Kushoto Ni Albert Peter (Mjumbe), Salim Amir (Mjumbe), Ahmed Hilal 'Aurora' (Mwenyekiti), James Mwinchande (Mjumbe) Na Julius Benjamin Mjumbe Pia Mara Baada Ya Kuchaguliwa Kwenye Mkutano Mkuu Wa Uchaguzi.

Ahmed Hilal 'Aurora'alichaguliwa kwa kura 52 kati ya wajumbe 55 waliojitokeza kushiriki uchaguzi huo. Wajumbe waliochaguliwa kura zao zikiwa kwenye mabano ni pamoja na Kweli Nahashon (48), Albert Peter (47), Salim Amir (42), Julius Benjamin (42) na James Mwinchande ambaye alipata kura 36.


Picha na Mashaka Mhando

No comments:

Post a Comment