BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, April 29, 2010

MPIGIE KURA BWANA MISOSI!!!!

Onyesha uzalendo wako kama wewe unatokea Tanga. Mpigie kura Bwana Misosi kwenye Kili Music Award ili wimbo wake wa 'MUNGU YUPO BIZE' upate kuchukua Tuzo ya wimbo bora wa Ragga. Misosi anachuana vikali na Dully Sykes (Shikide) Ambaye hivi karibuni alitangaza kujitoa, Drezzy Chief (Wasanii) pamoja na Benjamin wa Mambo Jambo (Fly). KUMPIGIA KURA:-andika kilim56 kisha tuma kwenda namba 15723

Tayari amekwisha achia kazi yake mpya mwaka huu wa 2010 inatambulika kama "HUWEZIJUA"akimshirikisha mtu mzima kutoka Calif...JUA CALI...

INTERVIEW YA STEVEN KANUMBA KATIKA LOVELY GAMBLE!!



Kwa mara nyingine tena ningependa kuwatolea Interview siku tuliyotembelea rasmi na World Service Radio katika studio zetu za Urban Pulse hapa UK tukiwa na Presenter Fred Ili kujadili Movie ya Lovely Gamble.

Pia aliweza kukutana na baadhi ya wanatimu wa Lovely Gamble na pia utapata comment za Steven Kanumba mwenyewe jinsi anaitwa siku hizi.

Wednesday, April 28, 2010

MISS CHUMBAGENI IJUMAA HII YA TAREHE 30/04/2010

APPLE PARTNERS GROUP
Inakuletea....

MISS CHUMBAGENI 2010

Lini: Ijumaa 30/4/2010


Wapi: Club la Tanzanite

Muda: Saa 2:00 usiku


Show!!!!!!!
Bwagamoyo SOUND Chini Ya Muumini Mwinjuma

'SIWAIMBII MADEMU ZANGU WA ZAMANI'- KASSIM



Siku chache baada ya gazeti moja kuchapisha habari iliyomhusu msanii mmoja kutoka katika kundi la Tip Top Connection Hemed Mganga a.k.a Cassim kuwa katika tungo zake amekuwa akiimbia wanawake zake wa zamani, ameibuka na kudai kwamba taarifa hizo si za kweli.

Kwa masikitiko makubwa msanii huyo amesema kuwa yeye hana marafiki wa karibu kiasi kwamba wanaweza wakajua A-Z kumhusu.

"Sina marafiki wa namna hiyo licha ya hivyo sina na sijawahi kuwa na msichana ambaye ana jina linalofanana na majina ya wasichana ambao huwa ninawaimba kwenye tungo zangu" alisema.

"Ujue siku zote muziki ni kama ufahamu wa mtu, na kile mtu anachokipenda, hivyo unapokuwa unaandaa tungo yanakuja majina mbalimbali kichwani na si kila msanii fulani anachoimba basi ni maisha yake halisi, hapana pale tunaelimisha na kuburudisha jamii na si vinginevyo" alisema.

Alisema kuwa akiwa kama msanii anatambua nini anafanya na mchango gani unahitajika katika jamii hivyo hawezi kufanya yaziyofaa.

Cassim amekana tuhumu zinazomkabili kuwa amekuwa akiwaimba wasichana wake ambao amekuwa na mahusiano nao hapo awali, majina yaliyotajwa kwenye orodha hiyo ni pamoja na Awena, Cindy, Amore.

Sunday, April 25, 2010

LET'S TALK ABOUT USAMBARA MOUNTAINS

The Usambara Mountains are a mountain range in North-East Tanzania, approximately 70 miles (110 km) long and ranging from 20 to 40 miles (30–60 km) in width. Mountains in the range rise as high as 8,000 ft (2,440 m). They are part of the Eastern Arc Mountains which stretch from Kenya through Tanzania, and are one of the world’s Biodiversity Hotspots.The range is accessible from the towns of Lushoto in the west, and Amani in the east. The Usambaras are commonly split into two sub-ranges, the West Usambara and the East Usambara. The East Usambara is closer to the coast, receives more rainfall, and is significantly smaller than the west.

Geology and Ecology:

The Usambaras are fairly unique in that, being in East Africa, their unspoiled regions are covered in the tropical forest which today remains mainly in the west of the continent. The mountain range was formed nearly two billion years ago and due to a lack of glaciations and a relatively consistent climate, the rainforest has gone through a long term and unique evolution resulting in an impressive amount of endemism and an old growth cloud rain forest. (Lovett 1993) West and East Usambaras, are large ranges of Precambrian metamorphic geologic formations of acid-geneses pyroxenes and amphiboles. These mountains were formed by faulting and uplifting creating the drainage system of troughs which form many watersheds which provide water to a majority of the population of northeast Tanzania. (Lundgren 1980)

Considered tremendously significant ecologically, there are many protected zones throughout the range which are being expanded and contributed to by the Tanzanian government, associated NGO's and research teams, and donor countries such as Norway. Several species are endemic to the Usambara forests, including the Usambara Eagle-owl (Bubo vosseleri), the Usambara Akalat (Sheppardia montana), the Usambara Weaver (Ploceus nicolli) and the tree Calodendrum eickii.

Human History:

Historically the Usambara Mountains have been inhabited by Bantu, Sambaa, and Maasai people who were a mix of agriculturalists and pastoralists. In the late 18th century German colonialists came to the area bringing with them a mix of cash crops like lumber trees, coffee, tea, and quinine, and began designating forests as either reserves for water conservation or timber use. (Rogers 2009) They also brought a slew of new, western ideas which were in many ways diametrically opposed to traditional beliefs such as coexistence with the forest verses forest as a “separate wilderness.” (Korschun 2007) The result of colonialism was a massive change in the way forests were perceived in the community, and conversion of traditional agriculture to cultivating cash crops such as quinine, pine trees, bananas, corn, tea, and coffee.

Development and Tourism:

Today, the population of the Usambaras has one of the highest growth rates (about 4% compared to the national average of 2.1%), a staggering amount of poverty and highest densities of people in all of Tanzania (R. Matthews 2009). Most of the inhabitants are subsistence farmers and rely heavily on the forests around them for timber, medicinal plants, clearing for agriculture, and fuel wood (S. Kiparo 2009). Furthermore 70% of the original forest cover of the West and East Usambaras has been lost (Doggart 2005). Major land and forest degradation remain a pressing issue. However there are still many places that attract tourists looking for an adventure off the beaten path. These include the bustling trade town of Lushoto, the once popular German resortAmani Nature Reserve and farm, and Mazumbai University Forest which is considered the last example of a pristine forest in the East Usambaras.


Friday, April 23, 2010

TAZAMA JAMAA ANAVYOTOA SADAKA YAKE!!!



Kwa mtindo huu ufalme wa mbinguni lazima uonekane!

Thursday, April 22, 2010

NYIMBO MPYA KUTOKEA TANGA!!!


Nyimbo mpya zilizonifikia mchana wa leo kutokea jijini Tanga.

1: Tuna Bang Zaidi Yao (TMC) kundi jipya
2: Wajua Nakupenda (Sudi G ft Penu)
3: Amini Nakupenda (Dokta Leader)

Zisikilize hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA! Usikie wasanii wa Tanga wanavyokuja moto kwenye anga za muziki wa kizazi kipya.

TANGA FLAVA YAPIGA HATUA!!

Hatimae wasanii wa Tanga ambao wanafanya muziki wa Bongo Falva wamepata unafuu wa nyimbo zao kujulikana baada ya blog hii kuwatengenezea Playlist.

Sasa unaweza kusikiliza nyimbo za Tanga Flava kupitia Blog hii kwa kubonyeza wimbo wowote ule unaoutaka hapo juu palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA!

Hii itawasaidia wasanii wa Tanga kufahamika zaidi ndani ya Tanga, Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Tumeanza na nyimbo chache hapo juu lakini nyingi zaidi zinakuja.

Nyimbo ambazo zipo kwenye playlist ni Mr President (Roma), Asali Shubiri (Fady Dady), Njoo Basi (Mo Kweli ft Mkolini), Aisha (Bwi Bwax), Ulisema (Shomy Love ft Big Smart), Taswira (Mwandei), Samahani (Pete), Mungu Yuko Bize (Bwana Misosi ft Chegge), Kila Sehemu (Omega Boys), Masham Sham (Dr John), Niite Mimi (Mitago ft Timer), na Nenda (Pete ft Tanga Stars)

Sikiliza ladha za wasanii wa Tanga.



Wednesday, April 21, 2010

LEYLA TOTII 'NYOTA INAYOZIDI KUNG'AA JIJINI TANGA'

Mtangazaji wa redio Mwambao Fm ya hapa jijini Tanga Leyla Totii a.k.a Ngumi Jiwe akiwa katika pozz wakati kamera za Anko Mo zilipomnasa muda mfupi kabla hajaingia kwenye kipindi. Leyla anafanya kipindi cha Jipe Raha chenye kupiga muziki wa taraabu, kinachorushwa na redio hiyo.

Leyla Totii akiwa na msanii pekee kutokea jijini Tanga Matonya alipokuja kutembea nyumbani.

Hahahahaaa....ilikuwa ni kicheko tu- Hapa dada akiwa na Nassoro Makau ambaye ni mkurugenzi wa 5 Brothers Entertainment yenye kuandaa Miss Tanga.

TANGA TOWN LEO ASUBUHI!!!!!!!!!!!

Siku hivi Tanga vibajaji vimekuwa ishu...hapa ni maeneo ya Mabanda ya Papa.

Hapa ni maeneo ya Sigara, karibu na Down Town Hotel pamoja na ofisi za Hot Net.

Hapa ni stendi kuu ya mabasi...ukifika Tanga kuna Garden nzuri katikati ya barabara ya Taifa.

Picha hii niliipiga wakati nipo kwa gari...hapa ni maeneo ya barabara ya 17.

Njia ya kuelekea Sahare..hapa ni eneo la Mapanda Ya Papa.

Hapa ni kituo cha daladala cha Bangi...pia wafanya biashara wadogo wadogo hujipatia riziki zao kama unavyoona kwenye picha.

Tuesday, April 20, 2010

MAANDAILIZI YA MISS CHUMBAGENI NI MOTO!!!

Punde tu baada ya mashindano ya Miss Tanga kuzinduliwa, tayari waandaji wa miss vitongoji wameanza mchakato wa kuhakikisha wanapata warembo ambao wataingia moja kwa moja kunako kambi ya kumsaka mnyange wa Miss Tanga. Kitongoji cha Miss Chumbageni ni moja ya vitongoji ambavyo vipo kwenye mchakato huo ambapo juzi walikutaka kwenye ukumbi wa La Club Tanzanite kwa ajili ya maandalizi. Pichani Julieth Kulangwa ambaye ndie muandaaji mkuu wa Miss Chumbageni kupitia kampuni ya Apple Partners Group.

Align CenterMdau wa urembo jijini Tanga, Blandina Lukindo ambaye pia ni mtangazaji wa redio Mwambao Fm akiwa katika pozz wakati wa mazungumzo ya kuandaa Miss Chumbageni.

Warembo katika mjadala wa kutafuta vichuna wa Miss Chumbageni.

Mambo yalikuwa mazito lakini tamati ilikuwa nzuri. Tayari Miss Chumbageni ina warembo tisa ambao watapanda juu ya stage kuumana vikali siku ya Mei Mosi tarehe 1/may/2010 Jumamosi.

Mtangazaji mwengine wa Mwambao Fm dada Neema Inana akiwa makini kwenye kikao.

Dada Suzane Uhinga, mmoja kati ya waandaji wa Miss Chumbageni kutokea kampuni ya Apple Partners Group akionyesha tabasamu pana wakati wa kikao.

Swahiba wangu wa ukweli Bra A alikuwepo.

Hapa no Comment kwa Blandina Lukindo, sijui alikuwa anataka kurembua maana hata sijaelewa. Ila hako kabinti pembeni 'DOLE TUPU'

Monday, April 19, 2010

ZE DUDU AWA'DISS WATANGAZAJI NA MA'DJ'S

The Bongo Hip Hop Legend, Godfrey Tumaini ‘Dudubaya’ amezindua harakati mpya ya kuitetea Hip Hop na Bongo Flava pamoja na wasanii wake kwa kutoa CD inayoelezea kinagaubaga unyonyaji unaoendelea aliyoipa jina la Nguruwe.

In that CD, Ze Dudu a.k.a Baba Willy anawachana presenters & DJ’s ambao wanatajwa kuishi kimjini kimjini kwa mgongo wa wasanii ambao wanawanyonya.

Mbali na kuwadisi presenters & DJ’s hao, pia Dudu ametoa shut out kwa waandishi kadhaa ambao wanaheshimu taaluma kwa kutokuendekeza rushwa.

Kwa sauti kavu, pia Dudu amewagonga nyundo baadhi ya wana Hip Hop wanaojiita wanaharakati kwamba sifa hiyo haiendani nao kwa sababu ni wanyonge na hawajui kutetea haki.

“Mimi kuna ma-DJ wamegoma kupiga nyimbo zangu tangu mwaka 2006, miaka minne bado nipo. Sijaenda kuomba msamaha na ninaishi, sisi ndiyo ma-legendary wa huu muziki, tumetoka nao mbali halafu watu wanakuja kula kiulaini.


“Mtu unaimba Hip Hop unajiita mwanaharakati, siku mbili nyimbo zako hazichezwi redioni unakwenda kuomba msamaha, unapiga magoti, siku mbili!” Ze Dudu anasikika akigonga sauti ndani ya CD hiyo.

Akichambua umafia wa baadhi ya watangazaji na ma-DJ Bongo, Ze Dudu anamwaga kuwa kuna watu wameweka mkakati kwamba bila shilingi 500,000 hawaruhusu kupiga nyimbo redioni kitu ambacho ni sawa na unyonyaji.

“Hizo laki tano tano msanii atatoa kwa redio ngapi? Kwa uwezo upi? Halafu unatengeneza albamu kwa milioni 4, unakwenda kwa mdosi unalipwa milioni 2, msanii atapata nini?” Anahoji Ze Dudu na kuongeza:

“Mtangazaji anakupigia simu anakuuliza upo wapi? Unamjibu upo baa, baada ya dakika chache anakuja na wapambe, demu wake, wanaagiza vinywaji vya bei mbaya eti ‘bili’ yote juu yako msanii. Watu tuna familia, mimi mwanangu Willy anasoma International School.”

'MKIWA' NGOMA MPYA YA FADY DADY!

Msani kutokea Mkoani Tanga, Tanzania Fady Dady ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Mkiwa. Akizungumza na Blog hii muda mfupi kabla hajafanya mahojiano na kituo cha Radio Mwambao cha jijini Tanga, Fady Dady amesema kuwa wimbo huo umetengenezwa For Life Record ya Jijini Dar Es Salaam pale mitaa ya Kinondoni chini ya producer Kara Lee.

(Fady Dady na Mimi- Anko Mo)

Aidha msanii huyo ameileza Anko Mo Blogspot kuwa kwa sasa anaachia ngoma moja moja kutokana na kubanwa sana na masomo. Fady Dady yupo chuo kikuu cha Dar Es Salaam Mlimani akisimoea Political Science..hata hivyo Fady Dady amewahi kutamba na wimbo kama Moyoni Naumia pamoja na Asali Shubiri ambayo bado inafanya vizuri hadi sasa.

Fady Dady katika Pozz

Friday, April 16, 2010

MIKE TEE AINGIA SOKONI TENA!



Unakumbuka ngoma kama Niacheni, Sintobadilika, Je Utaipenda, Nampenda, Kama na nyengine kali za Mike Mwakatundu aka Mike Tee a.k.a The last King From Nyaluland, sasa yupo jikoni (Studio) akipika album yake mpya baada ya kimya kirefu.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na video ya wimbo wake mpya wa'I LOVE U' ambao mpaka sasa inaendelea ku-bang ile mbaya, amesema yupo ktk hatua za mwisho kurelease remix ya wimbo huo ambayo yenyewe itakuwa kwenye mahadhi ya Hiphop-Techno.

Hata hivyo Mike Tee hakusema album hiyo itamalizika lini. Amesisitiza wapenzi wake wawe tayari na ujio huo mpya.

NGOMA MPYA YA KASSIM- 'UMEBADILIKA'

Msanii kutoka kundi la Tip Top Organization Kassim ameachia ngoma mpya inayoitwa "Umebadilika" iliyotengenezwa pale Mj Record chini ya producer Makochali.

Thursday, April 15, 2010

BREAKING NEWS!!!!!!.......DULY NAE AJITOA TUZO ZA KILI!!

Msanii Dully sykes aka Mr Misifa nae ametamka rasmi kujitoa tuzo za Kili.

"Nimesema na nilishasema sitaki kuwekwa katika category yoyote ile ya KIli Music Award, sioni faida ya tuzo hizo, sijawahi kupata tuzo tangu nianze mziki, single 36 mpaka sasa kama Salome,Hunifahamu na nyinginezo kibao zilizobamba lakini cha ajabu hakuna hata moja nimepata tuzo.....ni bora nitoe single tu na wala hata album sitaki."

Hayo yalikuwa maneno ya Mr Misifa alipokuwa kwenye mahojiano na kituo kimoja cha radio. Dully alikuwa katika Category ya wimbo bora wa Ragga, ambapo alikuwa akichuana na wasanii wengine kama Bwana Misosi (Mungu yuko Bize), Drezzy Chief (Wasanii) na Benjamin wa Mambo Jambo (Fly)

Dully amekuwa msanii wa pili kujitoa baada ya T.i.d kujitoa wiki mbili zilizopita.

POLE BRA A KWA KUFIWA NA BABA!

Swahiba wangu wa ukweli Ally Mohammed a.k.a Bra A hivi juzi aliondokewa na baba yake mzazi. Pole sana ndugu yangu, muombe sana mungu akupe subra kwa kipindi hiki kigumu kwani kufiwa na mzazi ni jambo kubwa sana. Anko Mo Blogspot na wadau wote inakupa pole sana na tunakuombea salama hadi mwisho wa msiba.

Bra A hapa akiwa na Matonya hivi karibuni.

Wednesday, April 14, 2010

WASANII WA TANGA WANAWEZA- MANEKE!

Producer wa A.M Record Maneke alipokuwa akifanya Interview Breeze Fm Radio ya jijini Tanga kwenye kipindi cha Track To Track kinachorushwa na redio hiyo. Maneke amesema kuwa wasanii wa Tanga wana uwezo mkubwa wa kuimba na hivyo yupo tayari kufungua studio jijini humo na kufanya nao kazi.

Maneke na Dj Bob Nass
Aidha Producer huyo ambaye alishawahi kufanya kazi kunako studio za Mid Man Records, Dhahabu Records pamoja na Baucha Records ameongeza kuwa- pamoja na wasanii kuwa na uwezo mkubwa lakini wengi wao huangushwa na Ma'producer wanaofanya nao kazi.

Amir, Bob Nass na Maneke
Hata hivyo Maneke alisema wazi juu ya kumkubali Producer wa Huruma Record Andrew kutokana na kazi zake kuwa na kiwango cha ukweli. Amir ndio host wa kipindi cha Track To Track, wakati Bob Nass ndio Dj wa kipindi hiko.
Add Image

MTU SABA KUISIMAMISHA WANAUME HALISI BAADA YA KIMYA KIREFU!

Kundi la TMK HALISI limesaini mkataba na kampuni inayoitwa DLC ambayo inafanya biashara zake China na Tanzania, kampuni hii ambayo yenyewe ndiyo itasimamia kila kitu ikiwemo mambo ya promosheni kutafuta maonyesho ya nje na ndani ya nchi pia kusimamia mauzo ya kila kitu.

Kiongozi wa kundi hilo Juma Kassim Nature, amepata wakati mgumu sana kuchuja na kuchagua vichwa vinne atakavyo fanya navyo kazi ya kuunda TMK Halisi mpya yenye vichwa vitani akiwemo yeye...badala ya ile ya awali iliyokuwa na wasanii 12.

Walio chaguliwa kusaini mkataba huo ni DOLO, BABA LEVO,JB WA MABAGA FRESH,KG SON pamoja na Juma Nature mwenyewe.

Tayari kundi hilo linalodhamiria kurudi upya baada ya kufulia kwa muda wa kutosha katika anga ya muziki wa kizazi kipya,limeshafanya kazi inayoitwa MNATAKAJE? ambayo imeanza kusambazwa redioni tangu mwishoni mwa wiki iliyopita.

MISS PANGANI HIYOOOOO!

Usikose!
Ukumbi: Safari Lodge Annex
Siku; Ijumaa ya tarehe 21/May/2010
Kiingilio: 5,000 kwa viti vya kawaida
10,000 kwa V.I.P

Tuesday, April 13, 2010

NI VIZURI TUKAMKUMBUKA SHAABAN ROBERT!



This is a remix of poem by Shaaban Bin Robert and sung in Swahili by Dr Peter Oriato. Ni vizuri kuwakumbuka mashujaa wetu katika fasihi andishi wanaotokea hapa mkoani Tanga.

Shaaban bin Robert, also known as Shaaban Robert (1 January 1909 – 22 June 1962), was a Tanzanian poet, author, and essayist who supported the preservation of African verse traditions. He was born in Vibamba in the country's Tanga Region. Robert is thought of as a great Swahili thinker and writer in East Africa and has been called "poet laureate of Swahili" and the "Father of Swahili.

TANGA CITY LEO ASUBUHI!

Jengo la CRDB Bank, moja kati ya majengo yenye mvuto jijini Tanga.

Eneo la katikati ya jiji.

Hili ni eneo la Hostel karibu na kijiji cha 21. Hiyo barabara inaelekea Chumbageni.

Hiki ni kituo Bangi...ndio kinavyoitwa wadau. Pata picha riafande ripo kwenye gari halafu anataka kushuka kituo hiko, "Arroo konda, shusha hapo Bangi" haina pozz sio..?

Bandari House

Karibuni Tanga

Waliosema Tanga Raha hawajakosea!