1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.
2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwenye same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!
Kwa mwaka huu msanii huyo kupitia Top Band na wimbo wa ASHA alikuwa akichuana kunako tunzo ya Wimbo Bora wa Kiswahili kwa upande wa bendi, ambapo Machozi Band (Nilizama), African Stars Band-Twanga Pepeta (Mwana Dar es Salaam), FM Academia (Vuta Nikuvute) Extra Bongo (Mjini Mipango) zikiwa kwenye category moja.
No comments:
Post a Comment