BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, February 2, 2010

"ALBUM IPO TAYARI"- PIPI

Mwanadada anayefanya Kolabo pengine kuliko mwanamuziki yeyote yule wa Kike kwasasa Doreen Aurelian a.k.a Pipi ametanabaisha ya kuwa album yake iko tayari na soon wapenzi wake wakae mtaani kuisubiri.

Akiongea katika mahojiano maalumu Pipi alisema album iko tayari na ina jumla ya nyimbo 10 lakini akasema bado hajaipa jina album hiyo mpaka hapo atakapokubaliana na uongozi wa THT.

“Unajuwa niko chini ya THT ndio maana siwezi kuweka kila kitu bayana, pale kuna uongozi ambao ndio utakaoweka kila kitu wazi, kifupi ni kuwa album ipo tayari na ina nyimbo kumi ila jina ndio bado mpaka nitakapokubaliana na menejimenti ya THT” alisema Pipi

Zaidi akaongea yakuwa kwasasa soon ata-release single yake mpya inayokwenda kwa jina la Usinune ambao amefanya na mkali mwengine kutoka THT Barnabas ambaye alikula shavu nae kwenye songi lililowatoa la Njia Panda.

Alimaliza kwa kusema studio alizofanyia kazi ni Bongo Record, BHirtz, 59 Records na sehemu nyingine.

No comments:

Post a Comment