BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, February 12, 2010

MPANGO MZIMA WA FELLA KWA MWAKA 2010!

Meneja na mlezi wa kundi la TMK Wanaume Family Said Fella a.k.a Mkubwa Fella amesambaza maelezo na malengo yake kwa mwaka huu 2010 kwa kundi zima la watoto wa Kiumeni. Fella alisema kuwa malengo makubwa kwa mwaka huu kwenye briefcase yake ni kama ifuatavyo.

“Kwanza kabisa nitahakikisha naitangaza na kuiuza album ya Saidi Juma a.k.a Chege album yake aliyoitoa siku za hivi karibuni ya karibu kiumeni, pia nitasimamia kama ilivyo kwa Chege album ya kundi ya Wanaume Kazini.

Nitalipia album ya Qaswida ya Madrasat Islamiah pale nyumbani Mbagala, album ya Chege na Mh Temba ya Vita mbele lazima iuzike, nataka studio yangu ieleweke kwa kuitangaza zaidi na wanamuziki wengi kuja kurekodi kwa kuifanya ya kisasa zaidi, studio inaitwa Poteza Records, mwisho kabisa nataka kuwatoa watoto wadogo wa kiumeni walioko huku Temeke” alisema Fella.

Fella ni mdau mkubwa wa muziki wa bongo fleva ndiye anayesimamia kazi zote za kundi la TMK Family.




No comments:

Post a Comment