Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyekuwa miongoni mwa waliofanya vizuri shindano la Bongo Star Search (BSS) ya 2008, Rogger Lucas, ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu ,amerudi na kitu kipya chenye sura tofauti na tuliyoizoea.Tulizoea kumuona akiimba peke yake au akishirikiana na msanii mwingine (featuring) ila kwa sasa ameibuka na kikundi chake kipya kiitwacho MOTHERLAND. Bendi hii imesukwa nchini uholanzi chini ya udhamini wa bendi iitwayo ROOTS RIDERS yenye maskani yake huko huko Uholanzi lengo likiwa kuwasaidia wasanii kutoka Afrika katika fani ya Muziki.
Kwa habari zaidi bofya hapa


No comments:
Post a Comment