BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, February 10, 2010

STUDIO YA KIMATAIFA YAFUNGULIWA MWANZA!

Katika kuhakikisha kuwa wasanii wa Kanda ya ziwa wanabaki pande zile za Mwanza bila kutoka mkoani humo kwa kuanzisha Studio ya nguvu ya kurekodi.

Studio hiyo ambayo ina sifa zote za kuitwa studio ya kimataifa imefunguliwa pande za mitaa ya Rufiji Mkoani kwa Kamanda Rwambow ikiwa na dhana zote za kisasa kabisa ambazo mwanamuziki yeyote anaweza akarekodi kwasasa.

Wanamuziki wengi toka pande hizo za Rock City wamekuwa wakitoka Mkoani humo na kuja Kurekodi anga hizi za kwa Lukuvi (Bongo).

“Unajuwa niliona kuwa wanamuziki wengi Mwanza ni makini hivyo basi nikaona kwanini wasumbuke kila siku kwenda kurekodi Dar ndipo nilipopata wazo la kufungua studio hizi ili niwarahisishie na kweli lengo langu limetimia, sasa wanamuziki wakubwa na hata wale wadogo wataweza kurekodi hapa” alisema mmiliki wa studio hizo

Studio hiyo inakwenda kwa jina la ATP, wanamuziki wakubwa kabisa waliotokea pande hizo ni kama Fid Q, Mad Ice, PNC na wengine wengi.

Mpaka sasa wanamuziki waliokwisha kutengeneza nyimbo zao ndani ya studio hiyo ni kama Z-Anton, Bwana Misosi, Geez Mabovu, Chelea Man




No comments:

Post a Comment