Baada ya kilio cha wasanii cha muda mrefu..wengi wao wakilalamika kuwa tuzo za Kili Music Awards zimekuwa zikiendeshwa kienyeji,hatimaye kilio chao kimesika kwa waandaji wa tuzo hizo kufanya maboresho makubwa.
Meneja uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, ametangaza njia ambazo wameamua kuzitumia ili kuboresha tuzo za Kilimanjaro kwa mwaka huu ili kuondoa wingi wa malalamiko yanayokuwa yakizikumba kila mwaka.
Akizitaja njia hizo, Meneja huyo alisema kuwa nyingi ni zile ambazo wamekuwa wakikosolewa na baadhi ya wadau wengi wa muziki wa hapa nchini.
Kavishe alizitaja njia hizo kuwa ni pamoja na kuboresha namna ya kumpata mshindi, mipango endelevu ya uboreshaji, utaratibu wa upigaji kura, kuwahoji wasanii 20 waliochaguliwa, kupata maoni katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma na Mwanza.
Njia zitakazotumika ni watu kupiga kura kwa njia ya kutumia meseji (SMS), mtandao na magazeti, watatumia kampuni ya Deloutte ambayo imekuwa na uzoefu wa kuhakiki na kusimamia upigaji wa kura na wameekuwa wakifanya shughuli hizo katika tuzo za nchini Kenya za Kisima na zile za Grammy za nchini Marekani.
No comments:
Post a Comment