BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, February 2, 2010

PROPAGANDA YA FID Q MTAANI FEB 25!

Mwanahiphop makini Farid Kubanda 'Fid Q', anatarajia kuingiza kitaani albam yake ya pili inayokwenda kwa jina la Propaganda Februari 25 mwaka huu.

Kubanda alisema kuwa amekuwa kimya kwa muda mrefu hivyo alikuwa katika maandalizi ya albamu hiyo ambayo anatarajia itakuwa ya aina yake kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya.

Alisema kuwa albamu hiyo ina jumla ya nyimbo 18 ambayo ameirekodia katika studio mbalimbali ili kuchanganya ladha ya muziki.Kubanda alisema kuwa baada ya kuingiza albamu yake sokoni anatarajia kuanza kurekodi video za nyimbo mbalimbali zilizopo katika albamu hiyo.

Alizitaja baadhi ya nyimbo ambazo zipo katika albamu hiyo kuwa ni pamoja na Propaganda, Usinikubali Haraka aliyoimba na Matonya, Ripoti za Mtaani aliyomshirikisha Zahir Zorro, Mtaua Gem aliyomshirikisha Juma Nature, Juhudi aliyoimba na Bi. Kidude, Kila Siku aliyomshirikisha QJ, Wananiita King aliyomshirikisha Nailon wa Manzese Crew, na Mwana Malungi.

No comments:

Post a Comment