BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, February 3, 2010

"MAUMIVU YA MIAKA 10"- WAGOSI WA KAYA

Wakali wa kutoa vidonge vya ukweli katika kuleta chachu ya maendeleo katika Taifa Letu Wagosi wa Kaya toka hapa Tanga wamerudi tena kwa spidi ile ile kipindi hiki wakiwa na jiwe jipya linalokwenda kwa jina la “Maumivu ya miaka 10”.

Wakiongea na VIJIMAMBO VYA TANGA Wagosi wakaya kundi linaloundwa na wakali wawili, walisema huo ni moja ya ujumbe wao kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.

“Unajuwa ndio kipindi cha watu kudanganyika lakini sisi tuko karibu na wananchi tutawaweka sawa na kuelewa wapi pakwenda, tunajulikana kama wazee wa Displini basi tunaendelezea” alisema Mgosi.

Wagosi wa Kaya walijulikana zaidi kwa nyimbo kama Tanga Kunani, Trafiki, Kero, Wauguzi na nyingine nyingi.
No comments:

Post a Comment