BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, February 11, 2010

RACHEL MLAKI AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI!!

Miss Tanga City Center 2009 na pia Miss Tanga namba mbili kwa mwaka huo Rachel Mlaki, hivi juzi alifiwa na mama yake mzazi jambo ambalo amesema limemuweka katika wakati mgumu sana.

Rachel ambaye hivi sasa ni mwanafunzi wa chuo cha UDOM, yupo mkoani Kilimanjaro kwa kwa ajili ya kumalizia mazishi ya mama yake, ameonekana ni mtu mwenye majonzi kutokana na tukio hilo la msiba.

(Rachel akiwa na rafiki yake)

"Asante kaka, mama alitokewa na uvimbe kwenye mguu wakamwambia ni Cancer. Wajua hata siamini, leo ndio tumemzika na sijui hata nitaishijie. Nameomba Mungu aniongoze kwani kaniachia wadogo zangu wawiliniwatunze" alisema Rachel ambaye ni mdau mkubwa wa VIJIMAMBO VYA TANGA

(Rachel akiwa na mtangazaji wa Mwambao Fm Ally Mohammed a.k.a Bra A)

Anko Mo Blogspot inakupa pole sana dada yetu mpendwa Rachel kwa msiba uliokukuta, mshukuru Mungu sana kwani msiba hauna mmoja kwani imandikwa kuwa kila nafsi itaonja umauti. Pigana kuhakikisha unatakeleza yale ambayo mama amekuachia.



No comments:

Post a Comment