
Msanii wa kutoka katika kundi la Tip Top Organization la jijini Dar Es Salaam ambaye pia ni raisi wa Manzese Ahmad Ally a.k.a Madee anatarajia kutoa ngoma yake mpya kutokaa kwenye Album yake inayoitwa IT'S ALL ABOUT MADEE ambayo amemshirikisha Ngwear.
Kwa mujibu wa meneja wa kundi hilo Babu Tale ambaye aliipasha VIJIMAMBO VYA TANGA , ngoma hiyo inatarajiwa kutoka siku ya Jumamosi ya wiki hii ikiwa imetengenezwa pale Mj Record producer akiwa ni Makochali.
Wimbo huo utakuwa unaitwa "It's all about Madee' ambao umebeba jina la album.

Kundi la Tip Top Organization linasifika kwa kuibua vipaji vya wasanii hasa wa Bongo Flava ambapo hadi sasa linawashikilia wasanii nguli kama Keisher, Kassim, Tunda Man, Madee, na wengine kibao.
No comments:
Post a Comment