BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, February 9, 2010

LORD EYES APONEA CHUPUCHUPU MIKONONI MWA POLISI

Mwanamuziki toka kundi la Nako 2 Nako lenye maskani yake mkoani Arusha Lordeyez alimaliza weekend yake kwa misukosuko mara baada ya askari polisi kumtia pingu kwa nia ya kumpeleka kituo cha Polisi.

Timbwili lenyewe lilikuwa hivi, Lordeyez na mchumba wake mrembo Ray C walikuwa wameharibikiwa mitaa ya MK Bar maeneo ya Mwananyamala na Kinondoni, mara ghafla wakapita Polisi ambao walikuwa kwenye doria ya kawaida ndipo msela akastuka ghafla na kufunga kioo na hapo ndipo polisi wakastuka kujiuliza kulikoni.


Jamaa wakageuza gari na kwenda walipo wapenzi hao wawili na kuwakuta na kuomba kuwafanyia upekuzi ndani ya gari yao ambapo Lordeyez alitia ngumu na ndipo polisi hao walipomkamata kwa nguvu na kumtia pingu kisha kumpeleka kituoni kwa upekuzi zaidi.

Lakini bila kupata chochote polisi hao hawakuambulia kitu na kumwachia mshikaji huru.



No comments:

Post a Comment