BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, February 4, 2010

KAA CHONJO NA AINA MPYA YA WIZI WA MKONONI!!

Kumeibuka aina mpya ya wizi wa fedha kupitia simu za viganjani. Wizi huo ambao umesharipotiwa jijini dar na kuingizwa mjini na aina ya wizi huo ambapo wezi wametumia mwanya wa kusajili number za simu kama kigezo cha kuweza kuwapata ulaji.

Wizi wenyewe huwa hivi unapigiwa simu na watu ambao wanajidai wao ni ajenti wa kusajili number za simu toka kampuni fulani ya simu halafu wanakuambia uwape details zako kama vile ni watu wangapi unapenda kuwapigia mara kwa mara ili kuhakiki, sasa basi ukishawapa wao wanakwenda kwenye kampuni za simu na kudai warudishiwe line zao kama vile simu zao ziliibiwa.

Baada ya sakata hilo ndipo wanasubiri simu zako zinapoita wao huzikata na kutuma meseji ya kuomba watumiwe kiasi fulani cha pesa kwa madai kuwa watarudisha kama hivi “Nipo kwenye Kikao siwezi kuongea, hebu nitumie laki 1 nitakurudishia mara nitakapotoka hapa”.

Au anaweza kupokea na kudai mwenye simu katoka kidogo akirudi atampigia, au wakati mwingine watatumia ubabe kwa kudanganya mwenye simu hiyo ametekwa hivyo watume hela upesi ili aachiwe.


Kaa Chonjo usikubali kutapeliwa.
No comments:

Post a Comment