BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, March 2, 2010

'KAMAL' KICHWA KIMOJA VIPAJI KIBAOO!!

Anko Mo: Mambo vipi kaka

Kamal: Poa Mo, niaje na kazi mkuu..?

Anko Mo: Tunamshukuru mungu kaka, naweza kuzungumza na wewe kuhusu Maisha yako, upo wapi na unafanya nini sasa..?

Kamal: Yeah man, itakuwa poa!

Anko Mo: Vijimambo Vya Tanga, na wadau wangependa kujua historia yako na familia japo kwa ufupi.

Kamal: Mimi ni mtoto wa kwanza kwa baba na mama mmoja nikifatiwa na twin brother’s ambao wapo hapa wamemaliza st’marys high school mmoja akiwa nchini India anasoma chuo mmoja akiwa hapa Tanzania anasoma pia.

kwa upande wa mama yangu kuna kaka yangu wa kwanza ambaye ni Engineer yupo Ufaransa anaishi ana masters ameoa mkewe ni doctor wamesoma wote Algeria. Anafuata sis wangu ambaye anafanya biashara za kwenda nje.

Halafu mimi halafu wadogo zangu wawili mapacha
halafu mdogo wangu wa kike wa mwisho yupo darasa la pili huyu amefuata akili ya mama yangu ana akili sana darasani mpaka walimu wanamsifia.

Ila
mungu aliza roho ya marehem baba yake mahala pema peponi alifariki mwaka 2002 mwezi wa 6 kwa cancer ya ubongo. Mama yangu bado yupo hai ila na yeye namuombea kwa mungu apone cancer ameshamaliza matibabu.

kwa upande wa baba yangu kuna kaka yangu omy sydney nikilitamka jina hili kw wale waliokuwepo miaka ya 80 mpaka 90 watakuwa wanamjua alikuwa bingwa wa break dancer tanzania miaka hiyo pamoja na akina marehemu black moses na wengine kibao na vilevile alikuwa judge kwenye cheza Tanzania iliyokuwa inarushwa na chanel ten mwka jana.

Anafuata dada yangu ameolewa halafu dada yangu mwengine yupo u.k takriban miaka
17 sasa anaishi huko ameolewa anafuata dada yangu mwengine ameolewa anafuata kaka yangu yupo znz anaishi ameoa ni acountant na kaka yangu
mwengine halafu mie then wadogo zangu wawili twins halafu mmoja wa mwisho anaitwa aboubakar huyu ni mtundu sana wengi wanasema amefuata utundu wangu.hahahhahaha.

Usishtuke kuwa wengi hivyo ila namshukuru mungu ni kwamba wote tulikuwa tukisomeshwa vizuri na mahitaji mazuri tu
tukipata, nikaamua kwenda Kenya kusoma music(utayarisha wa muziki na matangazo na dj)

Nilisoma huko na huko pia nilikutana na wasanii wengi tu wakubwa kwasababu chuo ambacho nilichokuwa nikikisoma kilikuw na studio kubwa inayoitwa homeboyz na sisi wanafunzi tulikuwa tukipewa baadhi ya nyimbo za wasanii wakubwa wa uganda na kenya kuzifanyia mixing na editing na kutengeneza beat, kama vile Peter Miles, Bebe Cool, Prezzo, Mr Lenny na wengine.

Maisha ya Kenya yalikuwa magumu sana kwani baridi sana nairobi na nilikuwa napata tabu sana kwa vyakula kwasababu tofauti na huku tanzania. Ila kwa upande wa chuo i realy admire this girl aliyekuwa akisoma class moja na mie alikuwa mkenya Lilian alikuwa ana dredd halafu ni dj katika club jazz she was my best friend, pale chuo nilikuwa mtanzania peke yangu.

Baada ya hapo nikasoma na kurudi bongo nikiwa mambo mengi sana

nimejifunza nikiwa bado nipo home kabla sijaenda Kenya, nilikuwa na laptop ya mzee wangu nikaitafuat fruityloops mpaka nikaipata na kujifunza mwenyewe sikuwa na mtu wa kunifundisha.

Nilipofika kenya nikakuta kazi zangu nafanya kwa urahisi sana hata wale wanafunzi wakawa wanashangaa wengi wao walikuja pale hawajui lolote
nikawa nawapa darasa. Walimu walionifundisha kwa upande wa dj ni dj weesly ambaye aliwahi kuja Bongo kushindana na dj Bush baby, halafu kuna dj
Enruf na dj Don pamoja na dj Hassan. Kwa upande wa utayarishaji wa muziki na matangazo ni Alex, Njoroge na Msyokaa.

So niliporudi bongo nilikaa sana nikifanya kazi zangu chumbani home nikiwapa watu wasanii wadogo wadogo beat wakaingize vocal.kuna mshikaji wangu anaitwa ono namfeel mbaya na naamini ipo siku ntamtoa tu kwasababu anafanya hiphop sana na ni mkali sana

Anko Mo: Duh, hiyo iko poa sana kaka. Mara ya kwanza kukuona ilikuwa Tanga City mwana, ilikuwaje hadi ukafika pande hizi..?

Kamal: Tanga nilikuja mwaka 2008 na mara ya kwanza nilikutanishwa na mkurugenzi wa radio mwambao fm na akaniambia nije kupiga mzigo pale radio na kweli. Nilipofika nikawa napiga kazi kama producer, mtengenezaji wa matangazo ya radio na ya biashara, lakini nilikuwa sijui kama nina kipaji

cha kutangaza. Huyu mtu sitomsahau kwasababu kuna siku nilikuwa ofisini na tafsiri habari za nje kwa kiswahili ili nimpe aingie nazo kwenye kipindi chake jamaa anaitwa Julius Kamafa na nilipompa zile habari akaniambia mbona nina sauti ya kutangaza kwanini nisiingie kwenye kipindi lakini nilikataa kwa kuwa na hofu nitaongea nini.

Lakini akaniambia nitasoma zile habari za wasanii na kweli nilifanya vizuri sana na nikaendelea kutangaza lakini huku nikiwa nina piga mziki kama dj kwasababu kazi ya kupiga mziki nilianza tokea nikiwa nina miaka 12 katika sherehe mbalimbali pale home zamani sana, wakti huo Saigon huyu msanii alikuwa akija home kwetu tukiandaa party alikuwa ni rafiki wa uncle yangu. Saigon ananijua tokea nikiwa mdogo sana pamoja na(balozi dola soul)na stigo wa diplomats.

Nilikuwa dj mmoja ambaye ni hatari sana lakini unajuwa tena kwenye mkusanyiko wa watu lazima utamuona mwanadada mrembo na hapa ndipo
nilipokutana na mchumba wangu ambaye ndio mke wangu mtarajiwa Samira Hassan....alikuwa mtangazaji wa pale radio alikuwa akikimbiza mbaya ni
noma na tukaanza mahusiano na baadaye radio mpya ikafunguliwa inaitwa Breeze fm na nikawa mtu wa kwanza kuanza kazi mie na dj Jb (juma bakari) na tukapiga mzigo haswa, lakini baadaye ikabidi nirudi Dar kujiendeleza kusoma zaidi na sio kazi tu.


Anko Mo: Ni mambo gani ambayo ulikutana nayo kwa kipindi chote ulichokuwa Tanga...?

Kamal: Mambo mengi sana ambayo nimekutana nayo Tanga, kwanza tukianza na mziki wa Tanga haukuwi hautanuki ni mmoja mmoja sana tofauti sana na dar. Ukijaribu kuangalia wasanii ni walewale labda ameongezeka mmoja ama wawili tofauti na dar na pia mziki huu producer wanachangia kuudidimiza.

Nimekaa sana na Mr Ebbo pamoja na Andrew pale Huruma Records na Motika records ni ma'producer ambao wana vipaji sana na
wanajaribu kuunyanyua muziki huu lakini kuna baadhi ya maproducer wanawaangusha.

Anko Mo: kwanini unasema baadhi ya ma'maproduer wanawaangusha wasanii wa Tanga yetu..?

Kamal: Mie kwanza ni mtu wa karibu sana na ebbo na ebbo alipofungua studio yake walikuwa wakijaa wasanii wadogo wadogo wengi sana mpaka hapati nafasi ya kupumzika na wasanii hao walikuwa sio wote wenye vipaji walikuwa wanalazimisha. Ikabidi aongeze bei na kweli alipoongeza wale wazamiaji wote wakapotea, pia kwa Andrew hivyo hivyo, lakini kusema ukweli wasanii wa Tanga wengi ni vichwa ngumu hawaelewi.

Ukiwaambia kitu wanakuona ni nuksi niliwahi kukaa na wasanii flani walinifuata niwatengenezee beat na nikawafanyia hivyo ila nikawaambia kweli kwamba kwenye kundi lenu ni wawili tu hapo ndio mnajuwa kuimba nyie wengine wote wasindikizaji kwahiyo mjitoe wale wote wakaniona mie mbaya nikawaambia haya ila ukweli ndio huo huwa si mfichi mtu.

Kuna producer wengine hapo nawajua kabisa ambao wana vistudio vidogo wana wa record
wasanii hao wadogo na wanajuwa kabisa hawana uwezo wa kuimba sasa hao ndio wanaowaangusha ma producer wenye msimamo.

Anko Mo: Poa kaka...wewe kama Producer unauzungumizia mziki wa Hip Hop...?

Kamal: Kusema ukweli mimi ni mpenzi wa hiphop na si diss mziki mwengine na nimeshatengeneza beat za nyimbo nyingi za wasanii hapa lakini sipati faida
kwakuwa msanii anachukua halafu anakuzungusha sasa si deal tena na wasanii wakubwa.

Sipendi niwaharibie kuwachana live but sio siri
ilinirudisha nyuma kwasababu nilitegemea wao wangenitoa na mie kuwatoa but imekuwa kinyume wametoka na mie nimebaki nalia lakini la maana nafurahi naposikia beat yangu imetendewa haki na wimbo una heat, kuliko kama wangenidhulum halafu hawasikiki.

Tanzania kuna wasanii wengi sana nizungumzie Tanga kwanza, Matonya bado hashikiki hana mpinzani mpaka leo hii. Ebbo bado anazidi kuliteka soko inabidi wajiulize wasanii kwanini jamaa analiteka sana soko. Then Roma a new comer ambaye anafanya vizuri then walikuja TNG squard lakini wakasambaratika now Omega Boys wamekuja but kitu kimoja tu tatizo kubwa nimeliona Tanga ni wasanii wanapotoka hawapendi kuongozwa kila mmoja anafanya yale anayoyajua.

Kwa mfano omega walifanya vizuri ila baadaye wakaachia nyimbo kwa fujo nyingi mpaka ikawa kero hujui uisikilize ipi, nadhani wangesimamiwa na mtu mwenyeji kwenye Music Industry wangekuwa mbali. Wagosi wapo kimya kama kundi najuwa wamejipanga kwasababu wakongwe watabaki kuwa wakongwe tu.

Anko Mo: Mapinduzi ya mwaka 2010 kwako ni yapi...?


Kamal: 2010 ni mwaka ambao nimepanga kujihusisha na wasanii wakubwa wachache watatu tu ambao soon watu wakae kusikia nyimbo za ukweli kutoka kwa wasanii hao, na mazungumzo tayari na bado vitu vichache tu ili tuanze kazi. Nilifungua studio dar nikaifunga baada ya mie kwenda Tanga kufanya kazi but now bado sijaifungua sitegemei kuifungua leo wala kesho, ila nafanya kazi katika studio za watu pindi wanaponiita.

Anko Mo: Ni usumbufu gani unaoupata ukiwa kitaani..?

Kamal: Kuna muda naogopa sana kujulikana maana ni kero ama balaaa hahahahahahah. Sasa hivi bado nasoma nachukua information technology na soon namaliza nilianza mwaka jana.

Anko Mo: Vipi kuhusiana na Ma'produer wa Bongo

Kamal: Ma'producer wa bongo naowakubali? kwanza heshima zote lazma ziende kwa huyu mtu ambaye mpaka ikafikia kumuota kutokana na kazi zake. Na bila yeye sijui huu mziki ungekuwa wapi. Najuwa angekuwepo mwengine lakini sidhani kama angeuweka kama ulipo sasa hivi, huyu jamaa alifanya mabadiliko makubwa sana.

Kuanzia hiphop mpaka Bongo Fleva, kuchanganya vionjo mpaka vya Raggae kwenye hiphop na kutoa wasanii wengi tu. Nasema hivi muacheni P Funk aitwe Majani leo hii akisema anastaafu mziki basi sijui wasanii watakuwaje maana wasanii wengi wataumia ingawa kuna producer wengi wazuri lakini hapana huyu ni legendary wa hapa kwetu Bongo.

Anko Mo: wataje basi producers wengine wanaopiga mzigo wa ukweli Bongo...?

Kamal: Hahahaa wapo wengi tu kama Marco chali, Lamar....nawakubali sana wanaonyesha mchango wao. Hata hivyo Dunga alileta mapinduzi ingawa akaondoka lakini alileta mapinduzi na muda ambao alikuwa anahitajika sasa kutumika sana yeye akawa ndio anaondoka. Pia kuna Nah Real na wengine wengi pamoja na Mj na Hermy B.

Anko Mo: Man, swali la mwisho! Ni msanii gani unaowapenda Bongo..?

Kamal: Wasanii well umhh ni wengi sana ila nawapenda wasanii wenye mashairi ya ukweli sana kama vile Fid q, Fa, Stopa wa rhymes nawengine wengi tu Joh Makini na wote wakali Jay Mo, Chid Benz, Sugu, Imam Abbas na kwa style jamaa namfeel sana G nako sijui kama kuna mtu ana style tamu kama huyu jamaa.ni ya kipekee

Anko Mo: Poa Kamal, Anko Mo Blogspot inakitakia kazi njema zenye mafanikio ili upake kutimiza malengo yako

Kamal: Poa kaka, kazi njema na wewe, wape Hi wana wote wa Tanga. Nitakuja kutembea one day!

Anko Mo: Poa


No comments:

Post a Comment