BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, March 29, 2010

MKUU WA MKOA WA TANGA SAIDI SAIDI KALEMBO AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA ZAHANATI MPYA WILAYANI PANGANI

Mh mkuu wa mkoa wa Tanga meja jenerali mstaafu Saidi Saidi Kalembo akiweka jiwe la msingi kwenye jengo jipya la zahanati lililojengwa katika kijiji cha Kwa Kibuyu kata ya Kipumbwi wilayani Pangani hivi karibuni alipokuwa ziarani.

Mkuu wa mkoa akiwa katika uso wa tabasamu wakati akimalizia kuweka jiwe la msingi. Zahanati hiyo mpya imejengwa na kampuni ya upandaji miti ya Tanga Forest.

Mkuu wa mkoa akiwaeleza jambo wananchi wa kijiji cha Kwa Kibuyu punde tu baada ya kufungua zahanati hiyo.

Mapokezi yalikuwa mazuri, akina mama wakimpokea mkuu wa mkoa wa Tanga Saidi Saidi Kalembo.

Akiwa katika msafara huku akiongozwa na mwenyeji wake.

Mwenyeji wa mkuu wa mkoa Bi Zipora Pangani ambaye ni mkuu wa wilaya ya Pangani akimtambulisha mheshimiwa Kalembo kwa wananchi wa Kwa Kibuyu.

Mfanyakazi wa Tanga Forest Bi Anitha Ngailo akimpa mkono mkuu wa mkoa baada ya kumsomea risala muhimu juu ya zahanati mpya ambayo kampuni yake imejenga.

Bi Anitha akisoma risala kwa mkuu wa mkoa.

Wananchi wa Kwa Kibuyu wakiwa makini huku mkuu wa mkoa akisikiliza risala iliyoandaliwa na Tanga Forest.

No comments:

Post a Comment