BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, March 1, 2010

"WRONG NUMBER" WIMBO MPYA WA BARNABAS

Mwanamuziki anayekuja kwa kasi kwenye muziki wa kizazi kipya Barnabas ameachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la Wrong number akimshirikisha mwanadada toka Machozi Band Lina.

Akichonga hivi karibuni Barnaba ambaye anasema kuwa yuko katika maandalizi ya mwisho mwisho kumalizia album yake itakayojulikana kama “Njia Panda” huo utakuwa wimbo wake wa tatu kuachia toka katika album hiyo.

“Wrong number ni nyimbo inayozungumzia ugomvi wa simu baina ya mume na mkewe baada ya mume kukuta msg kwenye simu ya mkewe na mkewe kuikana hiyo msg, itakuwa nyimbo ya tatu toka kwenye album yangu niliyoipa jina la njia panda, wimbo ulionitambulisha kwenye game hili” alisema Barnabas.

Zaidi aliongeza “nyimbo imefanyiwa kwa Duke lakini asilimia kubwa ya vifaa nimepiga mwenyewe, ukisikia gitaa ujuwe ni mkono wangu mwenye” alimalizia kusema Barnabas



No comments:

Post a Comment