BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, March 26, 2010

TUSIKIMBIE VIKAO VYA BASATA- AFANDE SELE

Mfalme pekee wa mashairi ndani ya Bongo Flava, Seleman Msindi a.k.a Afande Sele amechana ujumbe maalum kwa artists wa field hiyo kuacha tabia ya kusepa vikao vya kujadili mwenendo wa game vinavyoendelea hivi sasa ambavyo kwa kiasi kikubwa vimekuwa vikijadili kuhusu umoja wa wasanii.

Msindi alisema hayo last Weekend muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao cha kujadili muziki huo ambacho kilihudhuriwa na nyota kiduchu.

“Jamaa wanatakiwa wafahamu kwamba hivi vikao vina umuhimu, hakuna wa kutusaidia kudai haki zetu kama sisi wenyewe tutashindwa kuwa na umoja... Nawasihi sana washkaji wasisepe, waje tuweke mikakati,” alisema Afande ambaye anapenda kuitwa Baba Tunda.

Members wa chama hilo, ambao tayari wameshajisajili BASATA ikiwa ni pamoja na kulipa ada hukutana kila wakati kujadili mambo mbalimbali ya muziki huo, lakini wasanii upcoming wamekuwa wakitia timu kwa wingi, huku masupastaa wakikacha kiaina.

No comments:

Post a Comment