BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, March 29, 2010

MISOSI NAE ATAJWA TUZO ZA KILI!

Baada ya msanii Roma kutokea Tanga kutajwa kwenye tuzo za Teen Extra za Clouds Fm. Mkoa wa Tanga umezidi kujidhihirishia kuwa upo juu katika anga za muziki baada ya msanii mwengine kutokea hapa kutajwa kwenye tuzo za Kili kwa mwaka huu.

Msanii huyo ni Bwana Misosi ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Mungu Yupo Busy ambapo hivi karibuni aliibuka na video kali ya wimbo huo. Misosi ametajwa katika kipengele cha kuwania tuzo bora ya wimbo wa Ragga kupitia wimbo wake huo wa Mungu Yupo Bize ambapo anachuana na wasanii wengine kama Dully Sykes (Shikide), Drezzy Chief (Wasanii) pamoja na Benjamin wa Mambo Jambo (Fly).

Kama wewe ni mdau wa muziki wa Bongo Flava kutokea Tanga, hakikisha Bwana Misosi anachukua tuzo hiyo ili watanga wote tupate cha kujivunia. Pia endelea kumpigia kura msanii Roma kupitia http://www.nipe5.com au bonyeza hapa kupiga kura kwa Roma.

No comments:

Post a Comment