
“Tatizo si BSS, Benchmark, Madam Rita wala majaji, tatizo ni wasanii wenyewe kwa sababu hawana uwezo wa kuandika na kuandaa nyimbo zao ili zikubalike. “Wasanii wanaposhiriki BSS, wanaimba nyimbo za watu, kwahiyo wanaonesha uwezo wao kwa kuimba tu, hivyo wanakubalika na wanapigiwa kura lakini kwenye kutunga hakuna.
“Hii ndiyo sababu Jumanne Idd (mshindi mwaka 2007), Misoji Nkwabi (2008) wameishia njiani, unaona hata Pascal Cassian (2009) bado hajasimama, angalau Peter Msechu (1st runner up 2009) anaokoa jahazi.

“Hilo tumeliangalia kwa mapana na mikakati ya BSS mwaka huu ni pamoja na kutafuta watu watakaowaandikia nyimbo washindi na kuwachagulia ala, kwahiyo baada ya shindano wataingia studio na kufyatua mawe yenye akili.”
No comments:
Post a Comment