BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, March 26, 2010

'TUNAMTAKA NACY SUMARI MWENGINE'- MWANSOKO

Mkurugenzi wa Maendeleo na Utamaduni toka Wizara ya Habari na Utamaduni Bwana Herman Mwansoko amesema ni wakati sasa wa Tanzania kuinuka na kufanya vyema kwenye mashindano ya urembo ya Dunia.

Akiongea na Wakala wa Miss Tanzania toka Mikoa yote 20 ya Tanzania,Bwana Mwansoko alisema ya kuwa Watanzania wamechoka kuwakilisha kila mwaka na sasa ni wakati wao wa kwenda kushindana.

Mwansoko aliitaka kamati hiyo kufanya kama ilivyokuwa miaka iliyopota pale mrembo toka Tanzania Nancy Sumari alipofanya vizuri kwa kuipeperusha juu bendera ya Tanzania kwa kutwaa taji la Mrembo bora wa Afrika.

“Serikali pamoja na jamii ya Watanzania wanatamani mno kuona washiriki wa Tanzania kwenye shindano la Dunia wanafanya vizuri na jambo hilo linawezekana endapo tu mawakala watatafuta washiriki wenye sifa na ubora wa uhakika ambao watachuana kumpata Miss Tanzania.” alisema Mwansoko.

No comments:

Post a Comment