BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, March 3, 2010

'ONE LOVE' WIMBO MPYA WA STEVE

Anaitwa Steve William Gambo au Steve wa R&B mkali anayekuja kwa kasi kwenye game la Bongo Fleva ameibuka na kudhihirisha kuwa mwaka huu amedhamiria kiukweli mara baada ya kuachia ngoma kali inayokwenda kwa jina la ‘One Love’.

Akiongea hivi karibuni Steve amesema ndani ya ngoma hiyo amemshirikisha mwanadada wa siku nyingi kwenye game ambaye kwa muda mrefu amekuwa kimya Dataz, Steve ambaye kwa mara ya kwanza alijulikana kwenye ngoma ya Mr Blue ya Tabasamu ameonyesha anaweza kweli na kufufua matumaini ya wakali wa R&B kwenye muziki wa kizazi kipya.

“Wimbo unaitwa Sogea karibu kama ulivyousikia upo ndani ya album yangu ambayo soon itakuwa mtaani kwani bado nyimbo chache tu, mpaka sasa nina nyimbo sita ambazo zimekamilika kila kitu, ndani ya album yangu utasikia vichwa kama Ngwea, Squuezer, Dataz na wengine wengi, kwahiyo wapenzi wa wangu wakae tayari kitu kitaanguka soon mtaani” alisema Steve.



No comments:

Post a Comment