BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, March 24, 2010

MAADHIMISHO YA SIKU YA KIFUA KIKUU YALIVYOFANYIKA PANGANI KIMKOA!

Mh. Mkuu wa mkoa wa Tanga Major General (Retired) Saidi Saidi Kalembo akifungua maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ambapo katika mkoa wa Tanga yalifanyika wilayani Pangani siku ya jana. Kauli mbiu ilikuwa ni TUTUMIE MBINU MPYA KUONGEZA KASI YA MAPAMBANO DHIDI YA KIFUA KIKUU.

Mkuu wa mkoa akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zipora Pangani.

Mkuu wa mkoa Saidi Saidi Kalembo akiwa anatoka jukwaani mara baada ya kutoa hotuba.

Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi Zipora Pangani akisema neno kabla ya kumkaribisha mkuu wa mkoa.
Viti vikipangwa vyema kwa ajili ya wageni waalikwa.

Kazi ikaanza kama hivi. Hao ni wapiga ngoma wa kikundi cha Atomic kutokea wilaya ya Pangani kata ya Bushiri, wakitoa burudani.

Kisha wakaingia wacheza ngoma. Ngoma za asili ndio zilikuwa kitovu cha burudani. Atomic Group wakisakata ngoma.

Bi Zipora ambaye ni mkuu wa wilaya, alishindwa kuvumilia. Akaingia kutunza.

Hapa ilikuwa juu kwa juu.
Wakatoka, nikajua kazi imeisha. Kumbe walikwenda kuchukua vibatari vya moto. Tazama mambo hayo- huyo dada wa mbele alitia fora!

Kiongozi wa ngoma hiyo ya asili akiongoza jahazi. Shamrashamra hizi zilifanyika kwenye uwanja mkuu wa stendi ya mabasi yaendayo Tanga.

Mkuu wa mkoa akisema jambo.

Mkuu wa mkoa na wenyeji wake.

Wa kwanza ni mbunge wa Pangani Mh Rished, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa, mwenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani pamoja na katibu wake kule mwisho.

Mh Rished mbunge wa Pangani.
Wananchi walijitokeza kuja kusikiliza ujumbe wa siku ya kifua kikuu duniani.

Shaabani Kizamba ambaye alikiwa Mc pamoja na kiongozi wake Bwana Semnangwa, ambaye ni afisa utamaduni wa wilaya ya Pangani.

Kizamba akiwajibika wakati shughuli zikiendelea.

Wanachini wajaribu kukwepa camera ya VIJIMAMBO VYA TANGA , haya tena jamani.

No comments:

Post a Comment