BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Wednesday, March 31, 2010

MADEE ASHINDWA KUSIKILIZA WIMBO WA 'PENDO'

Msanii wa kundi la Tip Top Organization Ahmad Ally a.k.a Madee ambaye hivi karibu alifiwa na mchumba wake anayejulikana kwa jina la Pendo, amekamilisha wimbo wa kumuenzi mpenzi wake huyo ambao ameupa jina la PENDO akiwa amemshirikisha Matonya kutokea Tanga!

Kwa mujibu wa meneja wake Babu Tale amesema kuwa wimbo huo umetengenezwa Tongwa Record na msanii huyo ameimba kwa hisia kali kiasi cha kufanya utoe machozi utakapousiukiliza.

Aidha Tale amesema kuwa punde tu baada ya wimbo huo kumalizika, Madee alishindwa kuusikiliza kutokana na machungu ya kuondokewa na mpenzi wake ambaye katika wimbo huo amedai kuwa maisha yake yatakoma.

"Ni kwamba alipo maliza kurekodi alishindwa kuisikiliza aliishia kulia na akaondoka mpaka mie nikaifuata jana studio" alimalizia Tale

No comments:

Post a Comment