BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Monday, March 15, 2010

MAZINGAOMBWE YALIVYOTAWALA UWANJA WA TANGAMANO JIJINI TANGA!

Ilianza hivi, kama utani vile pale uwanja wa Tangamano jijini Tanga. Huyu dada aliambiwa ashike hayo makaratasi yaliyozungushwa na mtu wa mazingaombwe.

Hapa mtu wa mazingaombwe akichanganya madawa yake.

Kilichotokea hapo ni vibiriti, alizirusha na kila mtu akawa anagombania

Mtaalamu wa mazingaombwe akizidi kurusha vibiriti. Duh ili kuwa balaa, nilijaribu kuwasha kweli moto ukatokea wadau.

Hapa ndio ikaja kuwa balaa, huyu mtoto alilishwa makaratasi karibu gazeti tatu. Mazingaombwe bwana mmh!!

Tazama mtoto wa watu alivyoshindiliwa makaratasi!! Hayo yaliyotokeza hapo nje ilikuwa ni kama robo tu, mengi alimeza.

Amini usiamini mdau..zilitoa pipi kibao! Tazama watu wanavyogombania.

Mtaalamu wa mazingaombwe akirusha pipi kwa watu. Zilikuwa pipi kweli jamani, lakini ndio mazingaombwe hayo.

Ilikuwa vurugu tupu uwanja wote wa Tangamano, watu walikuwa wakigombania pipi kama unavyoona hapo- wakubwa kwa watoto!

Hahaha..ilinifurahisha sana hii! Jamaa ambaye ni mtaalamu wa mazingaombwe alikuwa akifukuzwa huku na huko kwa ajili ya pipi alizokuwa akizirusha. Hii ndio Tanga jamani!

No comments:

Post a Comment