Kundi la Tip Top Organization, lipo mbioni kuingia studio kwa ajili ya kufanya wimbo wa pamoja ambao hapo baadae utaingia kwenye albamu yao moja itakayowashirikisha wasanii wote wa kundi hilo.
Meneja wa kundi hilo Hamisi Tale a.k.a Babu Tale amesema kuwa, ameamua kufanya hivyo ili kuonyesha upendo wa kutosha kwa wasanii wake ili mashabiki wa wajue kuwa wana upendo wa kutosha katika kukuza sanaa ya muziki wa Bongo Flava.
Pamoja na kundi hilo kusifika kwa kuibua vipaji kila kukicha lakini, meneja huyo amedai kuwa wimbo pamoja na albamu hiyo itawashirikisha wale wasanii wenye majina makubwa ambao wanatokea kundi hilo lenye maskani yake jijini Dar.
Wasanii ambao watakuwapo kwenye albamu hiyo ni Madee, Keisher, Tunda Man pamoja na Kassim. Kundi hilo linatarajiwa kukutana siku ya leo kwa ajili ya maandalizi ya albamu hiyo na kujua ni siku gani wataingia studio kwa ajili ya kurekodi wimbo wa kwanza. Baadhi ya nyimbo zinatarajiwa kufanyika katika studio za Mj Record na nyengine zitahanyika studio tofauti tofauti, alimalizia kusema Babu Tale.

No comments:
Post a Comment