BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Thursday, March 18, 2010

WASANII WENGI WA BONGO FLAVA NI MAJUNGU- Q CHILLAH!

Align CenterMwanamuziki mwenye vituko kwenye muziki wa Bongo Fleva Athuman Shaaban Katwila a.k.a Q Chilla ameibuka na kutangaza hata siku moja hatataka urafiki tena na wanamuziki wa kibongo.

Q Chilla aliyasema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Radio nchini kwa kuulizwa yeye kumtuhumu T.I.D kuwa anamroga hivyo kushindwa kufanya kazi zake vizuri, habari ambazo ziliripotiwa na vyombo vya habari siku za nyuma.

“Mi nasema sitaki urafiki na mwanamuziki hawa wanaoimba imba kwasababu wengi wao wana majungu na ni wanafiki, wamekaa kimbea mbea tu” alisema Q Chillah bila kufafanua anamlenga nani zaidi.

Hivi siku za karibuni kumekuwa na habari za kutokuelewana baina ya wawili hao ambao walikuwa wakiunda Band moja. Haya wadau wa muziki wa Bongo Flava- kwa mtindo huu tutafka kweli..?


1 comment: