Kiukweli nilikuwa na ndoto za kuja kufanya kazi clouds fm siku moja na kweli hiyo ndoto yangu imetimia, namshukuru Mungu sana kwani sio wote wenye kuomba na kupata. Ila kila mmoja amepangiwa muda wake wa kupokea. Nakumbuka nilipokwenda kwenye mashindano ya kumtafuta mtangazaji wa Tv pale viwanja vya Leaders Club na ndipo mimi nikapita na ndo ukawa mwanzo wa mimi kuingia hapa mjengoni.
Naamini uwezo wangu pamoja na elimu niliyokuwa nayo vilifanya nionekane....na hata nilipofika hapa mjengoni wakaniona kuwa ninafaa kwenye kuandaa vipindi yaani producer na kusoma matangazo pia.
Kwa sasa nipo kwenye kipindi cha Africa Bambataa ya Clouds Fm, nikisaidiana na mwenzangu Sofai Kessy huku nikiwa kama muandaaji na masidizi wa studio.
Zaidi ya hapo nashurkuru sana wale wote waliofanikisha mimi kuwepo hapa kwani najua safari yangu bado inaendelea, mungu ndie anayejua zaidi kuliko mrabiri yeyote. Hata hivyo nikiwa hapa Clouds nimeshatangaza kipindi cha XXL cha kina B dozen, na pia siku moja niliweza kuatangaza pamoja na Diva katika Ala za Roho.
Sitasahau nilipotoka kabla ya kufika hapa, si pengine ni Mwambao Fm Radio iliyopo Tanga. Pele nilifanya kazi za uhakika pia kuendesha kipindi cha Tanga Flava, pamoja na Hot Beat. Big kwa watu wangu wa Tanga City, Anko Mo Blogspot pamoja na wale wote niliowahi kufanya nao kazi.

No comments:
Post a Comment