BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Tuesday, March 23, 2010

MASOMO YAMPUMZISHA KEISHA JUKWAANI!

Hofu ya kudunda (kufanya vibaya) kwenye pepa yake ya kidato cha sita imemfanya msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini na mwanachama wa Tip Top Connection, Khadija Shaban ‘Keysha’ kuweka kando kidogo masuala ya muziki.

Msanii huyo bora wa kike katika tuzo za muziki za Kili, ni mwanafunzi wa Shule ya kimataifa ya Cambridge, akichukua masomo ya Historia, Jiografia na Lugha (HGL), anatarajiwa kufanya mtihani wake wa mwisho Juni mwaka huu.

Akilonga kwa njia ya simu katika kuhusiana na kutoonekana kwake kwenye majukwaa ya muziki, Keysha alisema kunatokana na kutingwa na masomo na hasa ikizingatiwa amebakiza miezi michache kabla ya kufanya mitihani yake ya mwisho.


“Nimetingwa sana na masuala ya kitabu, hivyo imenibidi niweke muziki pembeni, si unajua mshika mawili...hivyo mashabiki wangu wasihofu, nitakapomaliza mitihani nitaingia jukwaani kama kawaida,” alisema.

Keysha ambaye amejipatia umaarufu mkubwa tangu ajitose kwenye ulingo wa muziki wa kizazi kipya, ambako nyimbo alizotoa zimeweza kufanya vizuri, huku tayari akiwa ameishatoa albamu mbili, ‘Usinitenge’ na ‘Keysha’.

No comments:

Post a Comment