BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX
Photobucket

Friday, February 26, 2010

WIKEND NJEMA WADAU!

Funny Pictures

MWEKASU HOSTEL- HOSTEL YA KISASA JIJINI TANGA!

Ni Hostel ya kisasa iliyopo mkoani Tanga, Tanzania maeneo ya Chumbageni karibu na Tanga Hotel kwenye jengo la CMC Automibile Limited ghorofa ya kwanza.


Imeanzishwa mwaka 2007 hivyo ina uzoefu wa kutosha na inapokea wageni 45 kwa pamoja. Pia inatoa huduma ya chakula na vinywaji. Mwekasu pia inatoa huduma ya Chakula na vinywaji kwenye sherehe kama Harusi, Birthday, Semina, na shughuli nyingine za kimaendeleo. Tuna ukumbi wenye kupokea watu 35 kwa shughuli za mikutano, vikao vya harusi semina na shughuli za maendeleo.

Hii ni sehemu ya sebule kwa wateja wote.

Mwekasu Hostel pia inahamasisha watu kutembelea vivutio mbalimbali vya kitalii vinavyopatikana mkoani Tanga kama Mapango Ya Amboni, Amani Natural Reserve, Magofu Ya Tongoni, Hot Spring (Chemchem Ya Maji Moto), Mkomazi National Park, Saadani National Park, pamoja na Tanzania kwa ujumla.

Sebule kwa upande wa pili. Na upande wa kupatia chakula

Pia kuna vitanda Double kwa wale watakaofika kwa familia ama group. Kwa mawasiliano zaidi:

* +255713400730

* +255786730400

* +255718400203

* +255719000010



TAPA TAPA, SHIKIDE KUPIGWA LEO IBIZA NIGHT CLUB CASSINO

Dully Sykes akiwa na msanii mwengine kutokea Tanga Untouchable. Dully anatarajiwa kufanya show leo jijini Tanga kunako Ibiza Night Club Cassino, club mpya ya kisasa ambayo ipo maeneo ya Donge. Ngoma kama Tapa Tapa, Shikide na nyengine kali za msanii huyo utazisikia leo kwa kiingilio cha 3000/=

Hata hivyo Dully atasindikizwa na huyo mnayemuona hapo juu Untouchable ambaye hivi sasa anatamba na wimbo wake mpya 'BINADAMU' aliomshirikisha Kassim, umetengenezwa AM Record chini ya Producer Maneky. Wasanii wengine watakaokuwepo ni Bab Lee, Omega Boys pamoja na Dula wa Michano.

Anko Mo Blogspot itakuwepo pande hizo na itakuletea mpango mzima wa picha zote na VIJIMAMBO VYAKE

Thursday, February 25, 2010

INTRODUCTION TO SME-SMS HELPLINE KAZI KWAKO!

Okoa muda na gharama zako sasa!!

MITAA YA TANGA TOWN LEO ASUBUHI!

Hapa panaitwa Hostel, ni kituo maarufu sana! Mbele kuna garden ya Uhuru Park. Mara kwa mara watu huenda hapo kwa ajili ya mapumziko.

Hilo jengo linatazamana na viwanja vya Tangamano, viwanja ambavyo ni maarufu kwa soko huria na mikutano ya hadhara.

Hapa ni Majestic Sinema, jengo ambalo lilikuwa ni maarufu sana kwa kuonyesha movies hapo awali. Ila sasa sijui linatumiwa kwa shughuli gani..nisaidieni wadau!

Hii ni njia ya kuelekea Old Tanga Sec School, hili ni eneo la Hostel pia.




Wednesday, February 24, 2010

OMEGA BOYS KAMA KAWA SIKU YA IJUMAA IBIZA NIGHT CLUB CASSINO

Baadhi ya wasanii wa kundi la Omega Boys la hapa jijini Tanga, ambalo siku ya Ijumaa litapiga show wakiwa pamoja na Dully Sykes na Bab Lee kunako Ibiza Night Club Cassino. Kiingilio ni 3000/=.....huyo wa kati ni Kochas, aliyevaa suruali nyeupe ni Dulla Wa Michano pamoja na Dj wa Breeze Fm Radio Dj Bob Nass, hao wengine ni fans!



Tuesday, February 23, 2010

'SITAKI TENA LAWAMA, NIMEPATA MCHUMBA'- HEMED

Hemed Suleyman a.k.a Hemed kijana aliyetikisa jumba la project fame kwa mwaka juzi ameibuka na kutangaza kuwa amechoshwa na kesi za kutembea na wake za watu ambazo zinamharibia sifa yake na sasa ameamua kuoa na siku za hivi atamtangaza mchumba wake ambaye atakuwa mkewe mtarajiwa.

Akichonga na hivi karibuni ambaye kwasasa amejikita zaidi kwenye mambo ya filamu amesema amepokea lawama nyingi na kesi kibao kuhusu kutembea na wake za watu lakini sasa ndio utakuwa mwisho.

“Nimeshapata mchumba na soon nitamweka wazi kila mtu amjuwe, hizi kesi zisizoisha sizitaki tena, lawama mtaani ya kuwa natembea sijui na demu wa fulani au mke wa mtu nimechoka nazo, sana sana zinaniharibia sifa yangu tu kila kukicha” alisema Hemed.

Hemed ambaye alikuwa mmoja wa wakilishi kwenye lile shindano la kuibua vipaji la Afrika Mashariki maarufu kama Tusker Project Fame aliingia kwenye masuala ya mziki mwaka jana na kufanikiwa kutoa baadhi ya nyimbo ambazo zilitingisha kama NINACHOTAKA na ULISEMA, yuko chini ya kituo cha kukuza vipaji cha THT.



HAPA NDIPO DULLY ATAKAPOPIGA SHOW IJUMAA (26/02/2010)

Sehemu ya juu Ibiza Night Club Cassino, club mpya ya kisasa iliyopo jijini Tanga.

Hii ndio Dancing Floor, pakiwashwa taa za club utapapenda!!

Upande mwengne wa Ibiza Night Club

Kwa juu, zaidi ya hizo feni unazoziona- pia kuna AC kila kona na nufanya ukumbi wote kuwe na kipupwe cha kutosha.

Duly Sykes atakuja kupiga show siku ya Ijumaa ya wiki hii, sambamba na Bab Lee. Kutoka Tanga watakuwepo Omega Boys, Untouchable, Dula wa Michano na wengine kibao. Kiingilio ni 3000/=..............wahi ticket call 0715000106



Monday, February 22, 2010

MTANGAZAJI WA MWAMBAO FM 'LEYLA TOTII'

Akiwa katika pozz baada ya kutoka kwenye kipindi cha Jipe Raha chenye mahadhi ya Taarab.

Akiwa ndani ya studio za Mwambao Fm Radio hapa jijini Tanga, pembeni yake ni Benedict Kaguo- nae ni mtangazaji wa radio hiyo.


Saturday, February 20, 2010

Friday, February 19, 2010

'SIMUOGIPI MTU KWENYE GAME YA MUZIKI'- RAY C

Mwanadada wa siku nyingi kwenye game la muziki wa kibongo Rehema Chalamalia a.k.a Ray C ameibuka na kusema hata waje wasanii wangapi wa kike lakini anaamini hakuna kama yeye kamwe na hakuna atakayekuja kuyafikia mafanikio yake.

Ray C au kama anavyojulikana kwa jina lingine kiuno bila mfupa aliyasema hayo baada ya siku za karibuni kuibuka wasanii wengi wa kike na kila mmoja kujitamba kwamba yeye ni zaidi ya wengine wote.

“Unajuwa watu wakikuona umekaa kimya wanadhani labda unawaogopa au vipi?, hawajui hata mtu kuwa unafanya nini, ni kweli kwa kipindi kirefu nilikuwa kimya lakini nilikuwa nafanya mambo yangu mengine nje ya nchi ambayo hayahusiani na muziki kabisa, basi wameibuka wengi na kashfa kibao, sasa nataka kuwaambia ya kuwa inatosha, na rasmi wajuwe kuwa mwaka 2010 nitakuwa kimuziki zaidi” alisema Ray C.

Ray C akiongea kwa hasira alizidi kusema “Lakini mimi hakuna demu wa kunitisha hapa Bongo si kwenye muziki sehemu yoyote ile, mi muziki nimefanya kipindi kirefu sana na mpaka sasa hakuna anayeweza kujifananisha na mimi, hakuna ambaye ameweza kufikia kiwango changu bado nipo mbali sana ndio maana napata shoo nyingi hata nisipotoa kazi mpya, nyimbo zangu hazichuji ukisikiliza ‘Na Wewe Milele’ sasa hivi hapo ulipo lazima usisimke lakini ni ya miaka mingi.” alimaliza Ray C

Tazama hapo pembeni/kulia kwako upige kura nani mkali wa bongo flava kwa madadaa



ROGGER ARUDI NA TASWIRA MPYA YA MUZIKI!

Mwanamuziki wa Bongo fleva aliyekuwa miongoni mwa waliofanya vizuri shindano la Bongo Star Search (BSS) ya 2008, Rogger Lucas, ambaye alikuwa kimya kwa muda mrefu ,amerudi na kitu kipya chenye sura tofauti na tuliyoizoea.

Tulizoea kumuona akiimba peke yake au akishirikiana na msanii mwingine (featuring) ila kwa sasa ameibuka na kikundi chake kipya kiitwacho MOTHERLAND. Bendi hii imesukwa nchini uholanzi chini ya udhamini wa bendi iitwayo ROOTS RIDERS yenye maskani yake huko huko Uholanzi lengo likiwa kuwasaidia wasanii kutoka Afrika katika fani ya Muziki.

Rogger amewataka mashabiki wake kuwa wavumilivu kwani hivi karibuni anatarajia kuingia sokoni rasmi akiwa na bendi yake hiyo katika kumbi mbalimbali za starehe kama ambavyo bendi nyengine za Tanzania zimekuwa zikifanya.

Ameweka bayana kuwa bendi yake inaundwa na wasanii kibao wakiwemo wakongwe na chipkizi kama; Ozeey, Grace Matata, Njuu a.k.a Crista Bella. Kala Jeremiah, na wengine wengi. Kwa sasa msanii huyo anatarajia kutoa video ya wimbo uitwao JASHO LA UPENDO kabla ya kuanza kazi rasmi na bendi yake hiyo.

Kwa habari zaidi bofya hapa



UBABAISHAJI KILI MUSIC AWARD SASA BASI TENA!


Baada ya kilio cha wasanii cha muda mrefu..wengi wao wakilalamika kuwa tuzo za Kili Music Awards zimekuwa zikiendeshwa kienyeji,hatimaye kilio chao kimesika kwa waandaji wa tuzo hizo kufanya maboresho makubwa.

Meneja uzalishaji wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, ametangaza njia ambazo wameamua kuzitumia ili kuboresha tuzo za Kilimanjaro kwa mwaka huu ili kuondoa wingi wa malalamiko yanayokuwa yakizikumba kila mwaka.

Akizitaja njia hizo, Meneja huyo alisema kuwa nyingi ni zile ambazo wamekuwa wakikosolewa na baadhi ya wadau wengi wa muziki wa hapa nchini.

Kavishe alizitaja njia hizo kuwa ni pamoja na kuboresha namna ya kumpata mshindi, mipango endelevu ya uboreshaji, utaratibu wa upigaji kura, kuwahoji wasanii 20 waliochaguliwa, kupata maoni katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Mbeya, Dodoma na Mwanza.

Njia zitakazotumika ni watu kupiga kura kwa njia ya kutumia meseji (SMS), mtandao na magazeti, watatumia kampuni ya Deloutte ambayo imekuwa na uzoefu wa kuhakiki na kusimamia upigaji wa kura na wameekuwa wakifanya shughuli hizo katika tuzo za nchini Kenya za Kisima na zile za Grammy za nchini Marekani.


YALIYOJIRI SAUTI ZA BUSARA HUKO ZANZIBAR!

Chid Benz kutoka Tanzania akiwa akilishambulia jukwaa kwenye Sauti za Busara huko Zanzibar.

Thandiswa Mazwai kutokea Afrika Kusini akionyesha miondoko ya kwaito ngome kongwe huko mjini Zanzibar

Mim Suleiman kutokea Zanzibar, akionyesha mambo ya pwani.

Dwada Jobarteh kutokea Gambia akionyesha umahiri wake jukwaani.



Thursday, February 18, 2010

KIVUKO KIPYA CHA PANGANI!! MAMBO SAFI SASA

Kivuko kilichokuwa kinasubiriwa kwa hamu kutokea wilaya Pangani kinaendelea vizuri kutokana na kuwepo kwa majaribio ya hapa na pale. Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited Boat Yard na M/S Johs Gralm Hossen A/S kutoka nchini Denmark, ndizo zinazosimamia ukarabati wa kivuko hicho.

Kilianza kutengenezwa May 10 mwaka 2009, na kimemalizika mwezi wa jana mwaka huu- kinatarajiwa kufunguliwa na mheshimiwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete panapo majaaliwa mwezi wa tatu.

Hapa kikiwa kwenye majaribio mchana wa leo



MENEJA WA TIP TOP ORGANIZATION 'BABU TALE'

Leo nimetumiwa wimbo mpya wa "IT'S ALL ABOUT MADEE" na meneja wa kundi la Tip Top Organization Hamisi Tale a.k.a Babu Tale. Meneja huyo amesema kuwa wimbo huo utabamba kutokana na mashairi pamoja na mindundo yake kuwa katika kiwango cha juu.

It's all about madee umetengenezwa kunako studio za Mj Record prodyuza akiwa Makochali. Ngwear ni msanii aliyepewa shavu kwenye songi hilo.



Wednesday, February 17, 2010

AMANI NATURE RESERVE- MOST BEAUTIFUL PLACE IN TANGA, TANZANIA

Amani Forest Nature Reserve, Located about 45 kilometers from Tanga Town, it is one of the most beautiful places in Tanga, Tanzania. Its one of the latest Nature Reserve established by the government to protect flora and fauna of east Usambara.

It harbors some of the animals only seen in Usambara such as Nduk eagle owl and most endemic plants. It was first established in 1902 as an agriculture research station by the Germans, and was turned into a nature reserve in 1997.

Amani Botanical gardens, the second largest botanical garden in the world lies in this reserve. Today the area continues to play a significant part in medical research hosting the Amani Medical Research Centre. The Nature Reserve has now been turned into an eco tourism attraction with greater emphasis on walking and hiking.

Walking and hiking through the forestry is the main attraction. Well-established walking routes are present. While walking you have an opportunity to see black and white colobus, blue monkey, and the nature's main attraction, Nduk eagle owl, a specie found only in Amani.

You will also see nine species of African violet garden flowers and colorful butterflies some of them found only in Usambara. Other birds include green headed oriole, Amani sunbirds, Uluguru violet backed, forest warbler. To sum up the area has wonderful birds, butterflies, animals and plants some of them found only in this area.




WAJUA CELEBRITZ WA TANGA CITY!!

Huyo dada anaitwa Asma Makao, na huyo kaka hapo anaitwa Nasor Makao- ni mkurugenzi wa Five Brotherz Entertainment ambayo imepewa dhamana ya kuandaa Miss Tanga.

Mshkaji anaitwa Roma, ni msanii wa bongo flava anayetokea Tanga City. Unakumbuka wimbo wa TANZANIA..? sasa hivi ana ngoma yake mpya inaitwa MR. PRESIDENT



Tuesday, February 16, 2010

HII NDIO CLOCK TOWER YA TANGA CITY!

Hii ndio Clock Tower ya Tanga City, ipo karibu na benki ya CRDB. Imejengwa na wajerumani mwaka 1901. Imekuwa kama kitambulisha cha mkoa wa Tanga. Karibu ujionee!


Monday, February 15, 2010

BORA MASHINE YA BIBI KIDUDE NI BALAA!!!

Jana wakati nipo ofisini, nilitumiwa wimbo mmoja na rafiki yangu ambaye ni mdau mzuri wa blog hii. Wimbo huo ni wa msanii Bibi Kidude unaitwa BORA MASHINE IWE NZIMA. Nitauweka uusikie hapa, ni mzuri ila mmmhh! huyu bibi ni kibokooo



HAWA WOTE NDANI YA IBIZA NIGHT CLUB CASSINO JIJINI TANGA

Msanii Dully Sykes akiwa na msanii mwengine kutokea Tanga Untouchable ambaye nae atapanda jukwaani siku ya Ijumaa ya tarehe 26/02/2010 kwenye ukumbi wa Ibiza Night Club Cassino uliopo maeneo ya Donge.

Mshkaji anaitwa J Coplo, mmoja wa wanafamilia ya Omega Boys. Nae atakuwepo siku ya show- jukwaa moja na Dully Sykes

Bra A, Untouchable pamoja na Kochas- wote hawa watakuwepo siku ya show.