BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, November 30, 2010

GAZETI LA THE CITIZEN LAITAJA 'VIJIMAMBO VYA TANGA' KUWA NI HOT BLOG

Kwanza napenda kumshukuru Mungu muweza wa yote kwa kuweza kutuamsha tena siku ya leo na kuendelea na majukumu yetu ya kila siku, ni yeye kwa mapenzi yake ndio amependa sote tuione siku ya leo....Pia nawashukuru wale wote ambao kila siku wanachukua muda wao kwa kupitia hii Blog, ni yenu na mimi nipo hapa kuwatumikia. Nachukua muda huu pia kuwashukuru gazeti la The Citizen kwa kuitaja Blog hii kuwa ni moja ya Blog zinazofanya vizuri nchini Tanzania.

Nafarijika kuona kazi ninayofanya inawagusa watu wengi. Tuendelee kufurahia Blog hii....inawezekana huu ndio mwanzo mzuri wa kupata Tuzo endapo litatokea shirika la kuandaa mashindano ya Blog zinazofanyakazi na kukubalika na wengi.

No comments:

Post a Comment