BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, November 25, 2010

TANGA OYYEEE!! MH. NUNDU AUKWAA UWAZIRI!

Mbunge wa Tanga mjini Mh. Omari Nundu hatimae ameitoa Tanga kimasomaso baada ya kuchaguliwa kuwa Waziri na Rais Jakaya Kikwete hapo jana wakati akitangaza baraza la Mawaziri.

Nundu ametajwa kuwa waziri katika wizara ya Uchukuzi, sanjari na naibu wake Mh. Athumani Mfutakamba.

Omari Nundu ni Mbunge wa jimbo la Tanga mjini, na aliibuka kidedea kwa jumla ya kura 40,225 na hivyo kuwabwaga wagombea wa vyama vya upinzani waliokuwa wakiwania jimbo hilo.

Kila la Kheri Mheshimiwa Nundu.


No comments:

Post a Comment