BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Wednesday, November 24, 2010

MIRIAM CHEMMOSS- NI KWELI ASILI YAKE TANGA

Endapo kuchanganya utaifa,damu na tamaduni mbalimbali ni mojawapo ya chachu za mafanikio fulani hapa duniani, basi ushahidi wa dhana hiyo unaweza kuupata kwa kuangalia maisha ya mrembo Miriam Chemmoss(pichani).

Miriam ni muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model) ambaye mpaka hivi leo ana haki ya kusimama na kujivunia rekodi yake katika ulimwengu changamani wa sanaa na maonyesho. Mwenyewe anasema safari yake ndio kwanza inaanza kwani bado ana ndoto na malengo chungu mbovu ya kutimiza. Hivi leo kazi zake nyingi anazifanyia kutokea jijini New York nchini Marekani anapoishi.

Kama ilivyo kwa wasanii wengi, safari ya Miriam katika ulimwengu wa sanaa inaanzia tangu akiwa mwanafunzi mdogo. Lakini ni pale alipohamia jijini New York mwaka 2004 na kujiunga na kundi maarufu lililojulikana kama The Marvallettes Revue lililokuwa chini ya Pam Darden, ndipo nyota yake ilipoanza kung’ara ipasavyo. Baadaye alijiunga na kundi lingine maarufu la Soukouss Stars kama mwimbaji pekee wa kike na mnenguaji kabla ya kuamua kuimba peke yake(solo artist) mwaka 2006.

Kwa upande wa uigizaji, Miriam ameshaigiza katika show mbalimbali maarufu ikiwemo ile ya “District” katika kituo maarufu cha televisheni cha CBS. Pia ameshiriki katika “Bedford Diaries” ya Warner Bros. Sauti yake imetumika katika matangazo mbalimbali ya biashara kama vile Western Union(USA-African Market) nk.

Kwa upande wa mavazi Miriam amewahi kuwa model wa jeans za Levi’s,Getty Images/Brazilian Salsa Club(Print),Bebe Noir Clothing Line,New York nk.Mwaka 2007 mtandao wa Jamati.com ulimtaja Miriam katika orodha yao ya Top 10 Sexiest African Women akiwa ni miongoni mwa wasichana wawili kutoka eneo la Afrika Mashariki.

Miriam asili yake kwa upande wa Mama anatokea kijiji cha Tingeni-Muheza, Tanga na pia marehemu bibi mzaa mama ni Mbondei kabisa. Ni faraja iliyoje Tanga kutoa msanii mkubwa kama huyu duniani. Kutaka kumjua vizuri Miriam tembelea website yake BONYEZA HAPA au kwa Facebook yake BONYEZA HAPA

No comments:

Post a Comment