BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, November 1, 2010

SEMKANDE WA CCM KIDEDEA UDIWANI PANGANI MAGHARIBI!!

Mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Pangani Magharibi John Semkande ameibuka kidedea kwa jumla ya kura 1126 dhidi Kitwana Sefu wa CUF aliyepata kura 589. Matokeo hayo ya awali yaliyobandikwa hivi punde yamedhihirisha wazi kuwa Semkande ndie kinara wa kata hiyo iliyokuwa na upinzani wa aina yake.

Hata hivyo jumla ya kura zote ni 1736 huku kura zilizoharibika ni 21. Tayari hadi sasa CCM inaongoza kata 11 kati ya kata 13 ambazo ni jumla ya kata zote za jimbo la Pangani. Endelea kufuatilia matokeo haya- nitakuwa nayaweka kila wakati kutegemea na matokeo ninayotumiwa na wadau.

No comments:

Post a Comment