BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, August 12, 2010

BAADA YA 'MACHO KODO' DR LEADER SASA KUJA NA 'KAGOMA KWENDA'

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Lucas Silas "Dr.Leader" amewataka mashabiki wake wakae tayari kwa ajili ya ujio wake mpya na wimbo wake mwengine ambao unakwenda kwa jina la "Kagoma Kwenda" anayotarajia kuiachia hivi karibuni.

Msanii huyo ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake Macho Kodokodo ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio hapa nchini,na Kueleza kuwa na wimbo huo ambao anatarajia kuuachia utakuwa mzuri zaidi.

Akizungumza na blog hii Dr.Leader alisema kuwa kwa sasa anacho angalia ni kitu gani ambacho mashabiki wake wanakuwa wanakiitaji ili kuweza kuwaridhisha pia kuweza kutambilika kimataifa kupitia mziki huo.

Dr.Leader alisema kuwa wasanii ambao ni chipukizi hawapaswi kukata tamaa hivyo waendeleee kufanya kazi zao vizuri na kwa kuzingatia maadili ya kazi zao pamoja na kujituma ili waweze kutambulika na kupata mafaniko.

Msanii huyo pia alielezea kuwa changamoto zinazowakabili wasanii wa mikoani ni kutokuwa na watu ambao wanakuwa wakiwasapoti katika kazi zao hivyo kuufanya mziki huo kuwa mgumu kwa kwa wasanii wa mikoani.

Aidha pia aliwataka wasanii wa mikoani kuunda ushirikiano kama walivyokuwa nao kupitia katika kundi lao la (Tanga Music Campany) TMC ambalo kwa sasa ni hatari mkoani hapa. Unaweza kusikilia pia wimbo wa TMC hapo juu pembeni palipoandikwa SIKILIZA TANGA FLAVA HAPA- wimbo unaitwa "Tunabang Zaidi Yao"

No comments:

Post a Comment