BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, August 30, 2010

KALEMBO AWAASA NIDHAMU WAREMBO WA MISS TANZANIA!

Mkuu wa mkoa wa Tanga,Said Kalembo amewataka warembo wanaotarajiwa kushiriki katika kinyanganyiro cha kumsaka mlimbwende wa Tanzania(Miss Tanzania)kuwa na nidhamu wakati wa mashindano hayo.

Mkuu huyo wa mkoa aliyasema hayo wakati akizungumza na warembo hao katika halfa iliyofanyika katika ofisi za mkuu wa mkoa waTanga ikiwa ni ziara ya siku moja ya warembo hao mkoani hapa.

Alisema kuwa kwa sasa kila kitu ambacho kinafanyika na kupata mafanikio makubwa ni lazima liwe nidhamu hivyo kuwataka warembo hao kuzingatia nidhamu wakati wa shindano hilo.

Aidha alisema kuwa warembo hao kwa sasa wana mzigo mkubwa sana na mzigo huo ni kuhakikisha wanashiriki katika shindano hilo wakiwa na nidhamu ya hali ya juu na ni lazima wakubaliane na matokeo ya aina
yoyote yale.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwataka warembo kuelewa kuwa urembo ni ajira na kazi wala wasikatishwe tamaa na watu wanaosema kuwa ni uhuni kwa sababu uhuni ni hali ya mtu mwenyewe.

Kwa upande wake,Mratibu wa miss Tanzania ,Hashimu Lundenga alisema kuwa wamefarijika na mapokezi hayo na kusema kuwa Tanzania kwa sasa ipo juu sana katika suala la urembo kuliko nchi yoyote ile ya Africa.

Jumla ya warembo 30 wanaotarajiwa kushiriki katika shindano hilo walizuru mkoani hapa na ambapo walipata fuska ya kutembelea vivutio vya mapango ya Amboni(Amboni Calves) yaliyopo mkoani hapa. Katika kinyang'anyiro hicho mkoa wa Tanga unawakilishwa na Jally Murei.

No comments:

Post a Comment