BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Monday, August 9, 2010

WAJUE WAREMBO WALIOUPA HESHIMA MKOA WA TANGA KWENYE SANAA YA UREMBO!!

Mona Koja

Kwa kuwa sanaa ya urembo nchini inazidi kuchukua nafasi, nimeona leo mpate kuwafahamu wanyange kutokea mkoa wa Tanga ambao waliwahi kufanya vizuri katika ngazi ya Kitaifa kwenye mashindano ya Miss Tanzania tangu yalipoanzishwa rasmi. Mrembo wa kwanza kushika nafasi ya juu kabisa ambaye anatokea Tanga ni Mona Koja, yeye aliwahi kushika nafasi ya tatu (3) Miss Tanzania kwa mwaka 1996. Ingawa Rekodi hiyo ya aina yake mpaka sasa bado haijavunjwa na mshiriki yeyote kutoka mjini hapa, imani kubwa ipo kuwa Tanga Tunaweza.

Ingawa Mona hakuvikwa taji la Miss Tanzania, lakini alileta upinzani mkubwa katika mashindano hayo mwaka huo na kufanikiwa kushika nafasi hiyo ya juu

Victoria Martin

Mrembo wa pili kutoka Tanga ambaye amewahi pia kushika nafasi ya juu ni Victoria Martin, alishika nafasi ya nne (4) mnamo mwaka 2007 na pia alibahatika kuwa balozi wa Redds. Victoria pia aliitoa kimasomaso Tanzania pale aliposhika nafasi ya tatu kwenye mashindano ya urembo ya Miss East Africa yaliyofanyika disemba mwaka jana.

Nadya Ahmed

Mrembo namba tatu ambaye yumo kwenye historia nzuri ya wanyange waliopata kuupa sifa mkoa wetu wa Tanga ni Zena Kichwa, alifanikiwa kuingia Tano bora ya Miss Tanzania mwaka 2002.

Na mwaka 2008 Nadya Ahmed mrembo mwengine kutokea Tanga alifanikiwa kutinga hatua ya kumi bora.

Glory Chuwa

SWALI...Je kwa mtindo huu mashindano ya urembo mkoa wa Tanga yanapanda ama yanashuka..?? Mrembo wa mwaka jana 2009 bibie Glory Chuwa aliambulia patupu japokuwa nguvu nyingi zilitumika walau nae atutoea kimasomaso.


Anna Kiwambo

Mwaka huu 2010 anayeshikilia taji hilo ni Anna Kiwambo, je atarudisha heshima ya watanga katika sanaa hii ya urembo..? Mchanga wa pwani huo!!...mie simo!!


1 comment:

  1. umemsahau Zaina Daudi alikuwa pia kwenye 5 bora miss tanzania

    ReplyDelete