BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Thursday, August 12, 2010

MGOMBEA CHADEMA ATAMBA KUVUNJA REKODI YA CCM TANGA!

Mgombea Ubunge Jimbo la Tanga Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kassim Makubeli, ametamba kuibuka na ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka huu na kuvunja rekodi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuliwakilisha jimbo hilo tangu uhuru.

Makubeli, ambaye kitaaluma ni mwalimu, alitoa tambo hizo hivi karibuni, baada ya kuwabwaga makada wenzake wawili katika kinyang'anyiro cha kuwania tiketi ya Chadema ya kugombea ubunge jimboni humo.

Aliwapongeza wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya kwa kumpitisha na kuwahakikishia kuwa hawatajutia kura zao akisema atahakikisha anavunja rekodi ya CCM ya kuliwakilisha jimbo hilo kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

“Ndugu zangu hamkukosea kunipa mimi kura….Kura zenu nitazitumia vema kwa kubatilisha hatimiliki ya CCM iliyojipa ya kuongoza milele Jimbo la Tanga…kuanzia sasa ni kazi kwenda mbele. Hakuna kulala mpaka kieleweke,” alisema Makubeli na akishangiliwa na wajumbe wa mkutano huo, uliofanyika katika Ukumbi wa Mkataba, jijini hapa.

Hata hivyo, alisema ushindi wake hautatokana na wanaChadema pekee na kwamba, kila mwanamaendeleo wa Tanga, anaamini atampa kura yake bila kujali itikadi za vyama vyao.

No comments:

Post a Comment