BLOG HII IMEDHAMINIWA NA: MWEKASU HOSTEL, PWEZA NIGHT CLUB TANGA, SOPHIA PRODUCTION, AFRICAN DESIGN, BREEZE FM, PANGANI COAST CULTURAL TOURISIM PROGRAMME, NA SAFARI LODGE ANNEX

Tuesday, August 17, 2010

LE GRAND LACASA CHICA YAFUNGWA KUPISHA MWEZI MTUKUFU!

KLABU maarufu ya usiku Mkoani Tanga Le Grand Lacasa Chica ambayo imefunguliwa hivi karibuni baada ya matengenezo makubwa imefungwa tena kupisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Klabu hiyo iliyoko Mtaa ya Indepence kati kati ya Jiji la Tanga imefungwa na kusitisha burudani hadi hapo mwezi mtukufu utakapomalizika.

Akizungumza na blog hili,Mmiliki wa Le Grand La Casa Chica, Hamisi Kindoroko alisema licha ya kuifungua klabu hiyo siku za karibuni baada ya matengenezo makubwa uongozi umeamua kuifunga ili kuwawezesha wateja wao kushiriki kikamilifu kwenye ibada.

Aliongeza kuwa baada ya kukamilika mwezi mtukufu Klabu hiyo itafunguliwa tena katika sikukuu ya Eid El Fitri.

"Tumeamua kufunga ili mwezi mtukufu upite baada ya hapo tutaendelea na burudani kama kawaida"alisema Kindoroko.

Aliongeza kuwa baada matengenezo yaliyofanyika kwa sasa yameifanya Klabu hiyo kufikia viwango vya kimataifa na kuendana na Hadhi ya Jiji kwani Tanga kwa sasa Jiji.

No comments:

Post a Comment